Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA LEO , HABARI ZA MICHEZO - Z'bar Heroes yafa na tabasamu. Rwanda na Sudan zapeta nusu fainali

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter


*Yapigwa 2-1 na Rwanda
*Sudan hiyoo nusu fainali baada ya kuilaza Burundi 2-0

SHUTI lililopigwa nje ya eneo la hatari dakika ya 86 na mshambuliaji nyota wa timu ya Taifa ya Rwanda 'Amavubi',
Kagere Meddie lilizima ndoto za Zanzibar 'Zanzibar Heroes' kucheza nusu fainali ya Kombe la Chalenji kwa kuiwezesha timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Mchezo huo uliokuwa wa kusisimua na wa aina yake kutokana na kiwango kilichooneshwa na Zanzibar Heroes, ulipigwa jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kabla ya mchezo huo, ulitanguliwa na robo fainali nyingine ambayo iliwakutanisha timu ya Burundi iliyooneshana kazi na Sudan ambapo Sudan ilitinga nusua fainali kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Wachezaji wa Zanzibar Heroes hususani waliocheza katika safu ya ushambuliaji iliyoongozwa na Ali Badr, watajutia nafasi nyingi walizipata katika vipindi vyote lakini hawakuwa makini kukwamisha mpira wavuni.

Kipindi cha kwanza, Zanzibar Heroes walitawala mchezo kwa kiasi kikubwa kutokana na kucheza kwa kujiamini na kupigiana pasi zenye uhakika ambapo dakika ya 15, Badr alitoa pasi safi kwa Abdulhalim Humud lakini shuti alilopiha Humud lilitoka nje.

Zanzibar Heroes iliendelea kutawala mchezo hasa katika kiungo kilichokuwa chini ya Humud na kumpa wakati mgumu kiungo machachari wa Rwanda, Haruna Niyonzima ambaye hakuonekana kama anavyojulikana.

Pamoja na kubanwa huko, Rwanda ambayo ilikuwa kama simba mwenda pole, ilifanya shambulizi la kushtukiza dakika ya 38 na kupata kona ambayo ilizaa matunda baada ya Mugiraneza Baptist kufunga bao kwa kichwa akiunganisha mpira wa kona uliopigwa na Niyonzima.

Baada ya kufunga bao hilo, Rwanda ilionekana kama imeamka usingizi ambapo dakika ya 43, nusura Baptist afunge bao la pili lakini alichelewa kupiga kichwa mpira uliopigwa na Kagere kutokana na pasi ndefu ya Niyonzima.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na dakika moja baada ya mpira kuanza, Zanzibar Heroes walisawazisha bao lililofungwa na Abdulrahman Mohd dakika chache baada ya kuingia badala ya Suleiman Kassim aliyeumia akiunganisha krosi ya Juma Othman.

Baada ya kufunga bao hilo, timu hiyo iliendelea kuliandama lango la Rwanda huku kwa wapinzani wao wakionekana kuzuia zaidi na mbele kumuacha mshambuliaji wao Olivier Kalekezi ambaye katika mchezo huo hakuwa na madhara kutokana kuwekwa chini ya ulinzi na Nadir Haroub 'Canavaro'.

Zanzibar Heroes dhahiri walionekana kuwa na kiu kubwa ya kucheza nusu fainali tofauti na ilivyotarajiwa na mashabiki wengi, dakika 82 nusura Badr awainua mashabiki wake baada ya kukosa bao la wazi kwa kupiga shuti lililotoka nje akiunganisha pasi ya Mohd.

Mashabiki wengi wakijua timu hizo zitamaliza ubishi katika hatua ya matuta baada ya kuonekana zitatoka sare lakini, Kagere alibadili fikra hizo kwa kupiga shuti nje ya eneo la hatari lililotinga moja kwa moja wavuni na kumuacha kipa Mwadini Ali akiruka bila mafanikio.

Katika mchezo wa kwanza, mabao ya washindi Sudan yalifungwa na Amir Abdenabi dakika ya 40 kwa kichwa akiunganisha krosi ya Khalifa Nakhit na la ushindi lilifungwa na Mohamed Osman kwa shuti kali.

Dakika ya 64, Sudan ilipata pigo baada ya mchezaji wake Nagmeldin Abdallah kutolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kurudishia rafu na mwamuzi Ronnie Kalema kutoka Uganda alimtoa nje.

0 comments

Post a Comment