IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamechachamaa kufuataia taarifa ya kurejeshwa kazini Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo. Akiwasilisha hoja ya kuundwa kwa tume leo asubuhi Bungeni, Mhe. Zitto Kabwe alisema analiomba bunge kusitisha shughuli zote za kuijadili serikali na kuunda tume kuchunguza sakata na Jairo na kuomba ripoti ya mkaguzi mkuu wa serikali kuleta ripoti bungeni ili ijadiliwe. Hoja hiyo iliuungwa mkono na wabunge wengi akiwemo Mhe. Ole Sendeka (CCM) ambaye alisema bunge haliwezi kudhalilishwa. Akasema pia kuwa kwa uamuzi wa kumrejesha Jairo kazini na Katibu Mkuu Kiongozi, Philomon Luhanjo kusema hakuwa na hatia, imemdhalilisha Waziri Mkuu, MIzengo Pinda, ambaye alipopata taarifa hizo siku ya kwanza aliliambia bunge kuwa angekuwa yeye angemfukuza kazi ndugu Jairo. Tume hiyo mpya inatarajiwa kutangazwa rasmi mwishoni mwa wiki hii na itaanza kazi mara moja.
You Are Here: Home - HABARI ZA KITAIFA , HABARI ZA LEO - Wabunge wachukizwa na kurudishwa kazini Jairo. Waunda kamati ya uchunguzi
0 comments