Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KITAIFA , HABARI ZA LEO - Jairo apigwa STOP Wizara ya nishati na Madini

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

Habari toka Bungeni sasa hivi zinasema Rais Jakaya Kikwete ameamuru Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini  Bw David Jairo asiendelee na kazi hadi hapo baada ya uchunguzi dhidi yake wa kuchangisha pesa ili Bajeti ya wizara yake ipite ukamilike.

Hayo yamesemwa sasa hivi na Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda wakati akijibu swali la papo kwa hapo toka kwa Kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai Mh Freeman Mbowe, ambaye alitaka kujua kama Bw. Jairo ataendelea kuwa likizo ili kupisha mchakato wa uchunguzi huo utaofanywa na kamati teule ya Bunge.

"Jambo hilo limekwisha fanya Mheshimiwa Rais", alijibu Mh Pinda kwa utulivu na kwa kifupi baada ya swali hilo, huku wabunge wakishangilia kwa kugonga meza.

Hatua hii inakuja siku moja tu baada ya Bw. Jairo kuripoti ofisini kwa shangwe, ambapo wafanyakazi wa wizara walimpokea kwa vifijo, na wengine hata kusukuma gari lake hadi ofisini, aliporipoti mapema asubuhi.

Uamuzi wa kumrejesha kazini Bw Jairo ulipokewa kwa husia tofauti na kila kada nchini, wengi wakihoji sababu ya mhimili mmoja kati ya mitatu iliyopo (Serikali, Bunge na Mahakama) kuingilia mwingine, ikizingatiwa kamba sakata hilo liilianzia bungeni na wengi walihisi ingekuwa vyema Bunge lingelishughulikia hadi mwisho.

Bunge lililidhia kuundwa kwa kamati maalumu kuchunguza tuhuma hizo na inategemewa wajumbe wake watatangazwa kesho wakati wa kufunga kikao cha Bunge kinachoendelea sasa. Ripoti yake inategemewa kutolewa Bunge lijalo

0 comments

Post a Comment