Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KITAIFA , HABARI ZA LEO - Polisi watinga Ikulu kupeleka malalamiko yao

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Ukonga jijini Dar es Salaam, wanaolinda makazi ya viongozi mbalimbali wakiwemo wastaafu, wametinga Ikulu na kupeleka malalamiko yao kwa njia ya barua wakidai posho zao za mwaka 2006.


Katika madai yao waliyoyaandika kwenye barua hiyo ya Machi mwaka huu,(nakala tunayo), askari hao wamedai kuwa wameamua kulifikisha suala hilo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wasira wakiamini kwamba kilio chao kitasikilizwa kwani madai yao ni ya miaka mingi.


Wameeleza kwamba, awali waliwahi kulifikisha suala lao kwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Laurence Masha lakini hawakusikilizwa.


“Tumeamua kulifikisha kwa Waziri Wasira kwa vile yeye ndiye yupo katika wizara inayohusiana na uhusiano kwani viongozi wetu hawatimizi majukumu kwa watu wanaowaongoza,” alisema mmoja wa askari hao kwa sharti la kutoandikwa jina gazetini.


Sehemu ya barua hiyo inasema; “ Tangu mwaka 2006 hatujalipwa fedha zetu za operesheni mbali mbali za kuwalinda viongozi … ni kiongozi gani wa serikali au ni mbunge gani wa nchi hii anadai posho yake?”


Gazeti hili lilimtafuta kwa njia ya simu Kamishna wa Polisi, (Idara ya Utawala na Rasilimali), Clodwing Mtweve alipoulizwa juu ya madai hayo alikiri kuyajua na kusema serikali inayashughulikia malipo yao.


Naye Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Balozi Khamisi Kagasheki alipoulizwa ofisini kwake hivi karibuni alisema: “ Ni kweli wanadai na tutawalipa, siyo fedha za lindo tu tutakazowalipa bali hata za uhamisho na posho zingine, tutahakikisha tunaondoa kero hizo,” alisema Kagasheki.

0 comments

Post a Comment