Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KIMATAIFA , HABARI ZA LEO - Iran yaidungua ndege ya Marekani

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Iran imesema majeshi yake yameidungua ndege isiyokuwa na rubani ya Marekani iliyokiuka sheria za nchi hiyo za angani.Shirika la serikali la habari IRNA hapo jana liliripoti kuwa afisa mmoja wa kijeshi ambaye hawakumtaja jina, alionya kuchukuliwa hatua kali dhidi ya ukiukaji wowote wa anga za nchi hiyo na ndege za kivita za Marekani.Katika taarifa,jeshi la Marekani lililoko Afghanistan lilisema kuwa ndege hiyo huenda ikawa ni ndege yao ambayo wahudumu wake walisema walipoteza mawasiliano nayo wiki iliyopita wakati ilipokuwa ikisafiri kuelekea magharibi mwa Afghanistan.

0 comments

Post a Comment