Wabunge wa Viti Maalumu CCM, Ritta Kabati (Iringa),kulia, na Mary Chatanda (Tanga) wakifuatilia mkutano |
Kikao hicho ambacho kilifanyika jana katika ofisi za CCM mkoani hapa kuanzia majira ya saa nne, kilishirikisha wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM mkoa, Makatibu wa vijana wa wilaya za Karatu, Monduli na Longido pamoja na vijana nane (8) wa UVCCM toka wilaya Arusha, Arumeru, Monduli ambao wanadaiwa ndio walioongoza maaandamano ya Mei 19 mwaka huu kuhojiwa.
Hata hivyo tangu kuanza kwa kikao hicho wingu zito limeonekana kutanda baada ya Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha, James Millya kuhojiwa na kikao hicho kwa zaidi ya saa nne kikao ambacho pia kilidaiwa kuwa na wajumbe kutoka makao makuu ya CCM taifa.Baada ya mwenyekiti huyo kuhojiwa alitoka kwenye kikao hicho akiwa mnyonge ambapo alikataa kuzungumza na vyombo vya habari na kuingia ndani ya gari yake na kuondoka katika eneo hilo, lakini baada ya dakika chache mtandao huu ulimtafuta kwa njia ya simu ya kiganjani kutaka kujua kulikoni lakini ilikuwa haipatikani.
Aidha katika eneo la CCM mkoa, askari wa Jeshi la Polisi waliovalia kiraia na maofisa usalama walionekana kufanya doria za hapa na pale huku lango kuu likiwa limezingirwa na “mabaunsa” wanaodaiwa kutoka Morogoro jambo lililoendelea kuwapa hofu baadhi ya vijana wa umoja huo ambao walikuwa nje wakisubiri hatma ya mwenyekiti wao.
Kufuatia hali hiyo vijana wa umoja huo walionekana kuwa na jazba huku wengine wakiwa wamevalia sare za chama hicho wakiendelea kuwatia moyo wajumbe wa kamati ya utekelezaji ya UVCCM mkoa, makatibu kutoka wilaya tatu na baadhi ya wajumbe wanaodaiwa kuongoza maandamano Mei 19 mwaka huu.
Hata hivyo, katika eneo hilo baadhi ya wajumbe waliokuwa wakisubiri kuhojiwa walitishia kutokubali kuhojiwa mbele ya Katibu wa CCM mkoa, Chatanda kwa madai kuwa naye ni mmoja wa watuhumiwa kama wao, huku wakihoji pia kwanini kundi la pili lililoshiriki katika maaandamano ya kuwataka “mapacha watatu” wafukuzwe kwenye chama hawakuitwa kuhojiwa na kamati hiyo.
0 comments