Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - EU kuijengea serikali uwezo

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
JUMUIYA ya Umoja wa Ulaya (EU) imesema itaendelea kusaidia kuijengea uwezo Serikali ya Tanzania katika mapambano ya kudhibiti wahamiaji haramu na biashara za magendo kwa kuweka mfumo maalumu wa kulinda mipaka ya Tanzania na nchi za Malawi, Msumbiji na Zambia.
Hatua hiyo, imekuja baada ya kuongezeka kwa vitendo vya biashara ya magendo vinavyofanywa na wafanyabiashara wadogo na wa kati na kusababisha baadhi ya nchi kupoteza mamilioni ya dola za Marekani.

Utafiti wa Jumuiya ya Kimataifa ya Uhamiaji (IMO), umebainisha kuwa kati ya watu 17,000 hadi 20,000 wanaojihusisha na uhamiaji haramu ni watu wanaofanya bishara ya magendo kutoka Ethiopia na Somalia kwenda Afrika ya Kusini na nchi nyengine.

IMO kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imeandaa mradi huo wa kudhibiti mfumo wa taarifa katika mipaka ya Tanzania na nchi nyingine za Afrika (BMIS).

Akizungumza katika mkutano wa kujadili masuala mbalimbali ya uhamiaji katika nchi za kusini mwa Afrika, uliofanyika katika mji wa Windhoek, nchini Namibia mwezi uliopita, Katibu Mkuu Wizara vya Mambo ya Ndani ya Nchi Abdulwakil alisema; “Serikali ya Tanzania inafahamu kazi ngumu iliyonayo kudhibiti wahamiaji  na mipaka yake katika mapambano ya kudhibiti uhamiaji haramu.”

Kwa upande wake Balozi wa EU Nchini Tanzania, Tim Clarke alisisitiza nchi kujenga uwezo ili kubaini  mbinu mbalimbali zitakazotumika  kudhibiti mipaka ya nchi.
Tags:

0 comments

Post a Comment