Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KISIASA , HABARI ZA KITAIFA , HABARI ZA LEO - CCM, Chadema waungana kupinga mauaji ya Tarime

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
VIONGOZI wa Vyama CCM na Chadema katika vijiji vitatu vinavyozunguka eneo la mgodi wa dhahabu wa North Mara, wilayani Tarime,  wameamua kuweka kando tofauti zao za kisiasa na kuungana katika kupinga mauaji ya watu sita, yaliyotokea katika mgodi huo.

Viongozi hao kwa pamoja, wameishtumu serikali kwamba ndio  chanzo cha mauaji hayo yaliyofanywa na polisi.
Walisema  miili ya watu waliouawa katika tukio hilo kwa kupigwa risasi, isingezua mvutano kuhusu mahali pa kuziika kama Mkuu wa Wilaya ya Tarime, angefuata ushauri wao.

 Wakizungumza  jijini Dar es Salaam  jana, wenyeviti hao wa vijiji vya Nyangoto, Kewanja na Matongo,  mauaji hayo yametoa funzo kwa serikali kuhusu umuhimu wa kutazama upya mikataba yake kampuni za madini.

Walisema hiyo inatokana na ukweli kwamba mikataba hiyo, inawanufaisha zaidi wawekezaji kuliko Watanzania ambao pia wamekuwa wakiuawa ndani ya ardhi yao.Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyamongo, kwa kupitia tiketi ya Chadema, Tanzania  O'Mtima alisema wilaya hiyo haina mkuu wake.

Alisema kauli hiyo inatokana na kitendo cha kiongozi aliyopo wakana pale  walipompelekea taarifa kuhusu mauaji.
O'Mtima alisema hawatambui na kwamba wao si wafiwa ambao ndiyo waliopaswa kwenda kumuona.

Alisema wananchi walikuwa wanamtambua kuwa ni mkuu wao  wilaya kwa sababu amewekwa na serikali
lakini kitendo cha kuwakana na kufurahia mauaji, kimeonyesha sura kuwa hayuko pamoja nao.Alisema kufuatia hali hiyo, watu wa CCM na Chadema, wameamua kuungana ili kuikaba koo serikali.

Alisema serikali inataka kuyafanya mauaji ya Tarime kuwa ya  suala la kisiasa, jambo ambalo haliwezi kukubalika.

Alisema viongozi wa Chadema walikwenda Tarime  kama viongozi vivuli wa serikali na wanaotambulika kihalali, lengo likiwa ni  kutimiza wajibu wao wa kuwatumikia wananchi na wala si vinginevyo.

Mwenyekiti wa kijiji cha Matongo, Itembe Itembe kupitia tiketi ya CCM  alisema mauaji hayo yamewafanya wananchi wa Tarime, kuondokana na tofauti za kisiasa na kuungana katika kupigania haki.

Alisema mauaji hayo yanachangiwa na kitendo cha serikali kuwasikiliza zaidi wawekezaji kuliko wananchi wake.

0 comments

Post a Comment