Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KITAIFA , HABARI ZA LEO - Mdhamini wa Mbowe ajisalimisha mahakamani

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter SIKU chache baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kutoa amri ya kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe pamoja na mdhamini wake, Julius Isaya Magwe na kufikishwa katika mahakama hiyo, Magwe amejisalimisha rasmi leo mahakamani.

Mdhamini huyo amejisalimisha leo mapema asubuhi saa 5:15 asubuhi akiambatana na wafuasi mbalimbali wa Chadema sanjari na wakili wa upande wa utetezi, Method Kimomogoro.

Hata hivyo, wakati Magwe akijisalimisha Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu amesema kambi hiyo inapinga Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kukamatwa popote alipo kwa sababu analindwa na Ibara ya 100 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mahakamani hapo na wakili upande wa utetezi, Kimomogoro alisema awali mdhamini huyo alikuwa akihudhuria mahakamani siku zote, lakini hakuhudhuria juzi kutokana na sababu za ugonjwa.Bila kufafanua ugonjwa huo wakili huyo alisema mdhamini huyo alikuwa akisumbuliwa na maradhi na hivyo kushindwa kufika katika mahakama hiyo juzi.

Wakili Kimomogoro alisema baada ya kupitia upya faili la maelezo ya kesi hiyo mahakamani, alibani kuna kipengele ambacho Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Charles Magesa alikitumia kufuta amri ya kukamatwa kwa washtakiwa na wadhamini Mei 30, mwaka huu.

Alisema amebaini kwamba kipengele hicho kunawalinda washtakiwa na wadhamini wao na kwamba uamuzi uliotolewa juzi na Mahakam hiyo kwamba  Mbowe akamatwe unatia shaka.Alisema tayari amewasiliana na ofisi ya hakimu huyo na kulifikisha jambo hilo.

“Kuna kitu ambacho nimekuja kukibaini baada ya kupitia kwenye faili la kesi hii ambacho hakimu aliagiza kufutwa kwa amri ya kukamatwa kwa washtakiwa na wadhamini ambacho nimekuja kukithibitisha leo, sasa uamuzi wa kutoa amri ya kukamatwa alioutoa jana hakimu nahisi alipotoka,”alisema Kimomogoro.


Katika hatua nyingine Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi ndogo za bunge jijini Dar es Salaam alisema amri ya kukamatwa kwa Mbowe inakiuka mila na desturi za miaka mingi zinazohusu kinga, Haki na Mamlaka ya Bunge.

Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Kusini (Chadema) alisema iwapo Mbowe atakamatwa, Polisi itakuwa limethibitisha kwamba haipo kwa ajili ya kulinda raia bali kuwaonea na kwamba kama chama watachukua hatua zozote zinazofaa.

“Ibara ya 100 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 inatambua na kulinda uhuru na mawazo, majadiliano na utaratibu katika bunge."Uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano au mahakamani au mahali pengine, nje ya Bunge,”alisema.

Alisema uhuru huo wa kikatiba umetiliwa mkazo katika vifungu vya 5,6 na 11 vya Sheria ya Kinga, Mamlaka na Haki za Bunge ya mwaka 1988.Alisema vifungu hivyo vinakataza mbunge kukamatwa au kupewa amri ya kuhudhuria mahakamani wakati akiwa ndani ya eneo la Bunge au wakati Bunge limekutana bila kuwapo kwa kibali cha Spika.

“Kwa mujibu wa Erskine May, mwandishi maarufu wa mila na desturi za mabunge ya Jumuiya ya Madola, muda muafaka na wa kutosha umechukuliwa kwa ujumla kuwa ni siku 40 kabla na baada ya mkutano wa Bunge,”alisema.

Alisema wakati mahakama hiyo ikitoa amri ya kukamatwa, Mbowe alikuwa analindwa na kinga ya Bunge na kwamba ataendelea kulindwa na kinga hiyo kwa kipindi chote cha mkutano wa nne wa Bunge hilo.

Katika kupangua amri ya Mahakama, Lissu alisema Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inashangazwa na ubaguzi wa wazi unaoonyeshwa na Polisi dhidi ya Wabunge wa Vyama vya Upinzani.

0 comments

Post a Comment