Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA LEO - Msuya amshukia Makamba. Amtaka kujiuzulu

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
KADA wa (CCM)   David    Msuya Mkazi wa Kibaha mkoani Pwani amemshukia Katibu  Mkuu wa CCM Yusufu Makamba akidai  ameshindwa kukiongozi chama hicho na kumtaka ajiuzulu.  MwanaCCM huyo amesema Makamba ndiye chanzo cha kuibuka kwa migogoro na malumbano ndani ya chama hicho.

Msuya pia amewataka vigogo wa CCM, Umoja wa vijana (UV-CCM) na wanachama wote kuacha kulumbana kwenye vyombo vya habari akisema kufanya hivyo ni kukiua chama.

 Kauli ya Musuya imekuja huku chama hicho kikiwa kwenye mvutano kati ya baadhi ya vigogo wa CCM na UV-CCM. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana  Msuya  alisema kitendo cha katibu mkuu kuacha malumbano hayo yaendelee  ni hatari kwa chama na ni ishara tosha kuwa ameshindwa kazi yake, hivyo anasitahili kujiuzulu.

“Hebu tutazame wakati wa uongozi wa Benjamin Mkapa na katibu wake Phillip Mangula chama kilikuwaje, Katibu Mkuu aliwajibika na hivyo alionyesha kuimudu nafasi yake  ndio maana hata chama hakikuyumba ”alisema Msuya.

“Katibu wetu wa sasa ndio chanzo cha malumbano yanashika kasi ndani ya chama kwa sasa, yeye amekaa kimya, baada ya kutokea malumbano  ilimpasa kuwaita wote wanaolumbana nje ya utaratibu kwenye kamati ya maadili na kuwaonya”alisema Msuya.

Msuya alisema kitendo cha kuacha malumbano hayo kuendelea ni hatari kwa chama sababu kunaweza kutoa mwanya hata kwa baadhi ya wanachama kukihama na watu waliotaka kujiunga kuendelea kukikimbia. Alisema kwa sasa CCM pamoja na jumuiya zake si wakati w a kuendeleza malumbano na badala yake ni wakati wa kufikiri wapi walikiuka hata kusababisha kupoteza majimbo mengi kwenye uchaguzi mkuu uliopita.

Alisema kwa sasa viongozi walipaswa kukaa chini kupitia na kutafiti wapi walikotoka na wanakokwenda wakiweka malengo zaidi kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.  Katika hatua nyingine Msuya aliwataka makatibu wa chama hicho ngazi zote kuandaa na mikutano ya hadhara kuwezesha wananchi kukutana na viongozi ili kujadili chama chao.

0 comments

Post a Comment