Kaimu Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan amevunja baraza la mawaziri ikiwa ni mwezi mmoja tu tangu kuchukuwa wadhifa huo baada ya Rais Umaru Yar'Adua kusafiri Saudi Arabia kwa matibabu.
Wengi walikuwa wakimdhihaki kwamba hana uwezo wa kuongoza lakini huenda wameshangazwa na hatua yake ya kuvunja baraza la mawaziri.
Wiki iliyopita Bwana Jonathan alimfuta kazi mshauri wa maswala ya usalama wa nchi baada ya machafuko kuzuka katika mji wa Jos.
Baada ya kuwaachisha kazi mawaziri, kaimu huyo wa rais anahitajika kutoa orodha mpya kwa bunge la taifa.
Wachambuzi wa siasa wanasema huenda akatumia fursa hiyo kuwaondoa wandani wake Rais Yar'Adua ambaye bado anaumwa.
0 comments