Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa John Nchimbi, akitoka Mahakama Kuu Dar es Salaam jana, alipokwenda kutoa ushahidi wa kesi aliyoifungua ya madai ya sh1bilioni, gazeti la Tanzania Daima Kukia ni Kapteni John Komba shadidi wake na katika ni wakili wake Kennedy Fungamtama na . ASEMA MFUMO WA UCHAGUZI NCHINI UNACHOCHEA UFISADI |
MWANASHERIA Mkuu mstaafu wa Serikali Jaji Mark Bomani, ameandika waraka mzito kwenda CCM na serikali yake, ambao pamoja na mengine unaelezea mfumo wa sasa wa uchaguzi kuwa ni kichochea cha ufisadi katika kupata viongozi wa dola.
Waraka huo mzito wa Jaji Bomani ambao unazungumzia nchi ilikotoka, iliko na inakoelekea, umekuja kipindi ambacho joto la uchaguzi mkuu wa Oktoba likiwa juu.
Ndani ya waraka huo wenye kichwa cha habari: "Mapendekezo ya Mark Bomani, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mstaafu," ambao gazeti hili limefanikiwa kupata nakala yake jijini Dar es Salaam jana, Jaji Bomani amechambua mifumo miwili mikubwa ya uchaguzi ambayo ni nguzo ya demokrasi.
Katika uchambuzi huo, Jaji Bomani, alisema Tanzania kama makoloni mengine yaliyotawaliwa na Uingereza, imerithi mfumo wa uchaguzi wa majimbo wa mkoloni huyo, lakini una athari kubwa ikiwemo matumizi ya rushwa katika uchaguzi na gharama za kuendesha uchaguzi katika majimbo.
Jaji Bomani alifafanua katika waraka huo kwamba, pamoja na Tanzania kurithi mfumo huo unaotumiwa na nchi ya Jumuiya za Madola (Commonwealth Countries), hivi karibuni ilijiongezea aina nyingine ya uwakilishi kama vile viti maalumu.
Akichambua mfumo huo wa uchaguzi wa majimbo na kuulinganisha na ule wa uwiano wa kura (Proportional representation) unaotumika katika nchi za Nordic kama Sweden, Jaji Bomani alisema mfumo huo wa uwiano wa kura unapunguza gharama za kuendesha uchaguzi na hata vitendo vya rushwa katika kupata viongozi wa dola.
Ndani ya waraka huo, Jaji Bomani alifafanua kuwa pamoja na uzuri wa mfumo wa uchaguzi wa majimbo ambao unawezesha wapigakura kumchagua mgombea, kwa upande wa pili unamfanya mgombea atumie kila njia ili aweze kushinda, zikiwemo fedha chafu na vitu vingine.
Waraka huo wa Jaji Bomani umefafanua kwamba, fedha na vitu mbalimbali hutolewa kwa viongozi na wapiga debe na kuongeza: "Hivi karibuni hapa nchini ushawishi wa aina hii uliongezeka kwa kasi kubwa kiasi kwamba serikali imebidi ipitishe sheria ya kudhibiti dosari hii".
Jaji Bomani aliweka bayana kwamba, kutokana na hali ya rushwa katika uchaguzi ilivyofika pabaya, bado hakuna njia ya uhakika ya kuzuia hilo.
"Pamoja na jitihada hizo hakuna njia yenye uhakika ya asilimia mia ambayo itadhibiti vitendo vya rushwa na matumizi mabaya ya fedha, hasa katika nchi ambayo wananchi wake wengi ni maskini na uelewa wao wa haki zao ni mdogo," amesisitiza katika waraka huo.
Katika waraka wake huo Mwanasheria huyo anayeheshimika nchini, alitaja dosari nyingine ya mfumo huo wa uchaguzi unaotumiwa na Tanzania kuwa ni pamoja na kila jimbo linalofanyika kugharimu fedha nyingi kulitekeleza na kusimamia.
"Pakitokea nafasi ya kiti cha ubunge au uwakilishi katika jimbo inabidi uchaguzi mdogo ufanyike na zoezi lote, pamoja na gharama zake inabidi lirudiwe. Hii inasababisha gharama kuwa juu," alisema.
Jaji Bomani ameweka bayana katika waraka huo kwamba, hasara nyingine ya mfumo huo wa sasa ni pamoja na kuwepo shinikizo la kuongeza majimbo ya uchaguzi.
Alifafanua kwamba, tayari kumekuwa na shinikizo kubwa la kutaka kuongezwa majimbo, hatua ambayo ilimfanya hata Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Uratibu wa Bunge), Philip Marmo kutoa tahadhari kwamba, haiwezekani kuongeza idadi ya wabunge kwa vile hata nafasi katika ukumbi wa bunge mjini Dodoma zimejaa.
Jaji Bomani alikumbusha akisema:"Miaka ya nyuma wilaya nzima ilikuwa na jimbo moja tu la uchaguzi. Na kwa kiasi kikubwa uwakilishi ulikuwa sawa tu".
Ndani ya waraka huo, Jaji Bomani alihoji juu ya kuongeza majimbo kwa kisingizio cha idadi ya watu na akitoa mfano kitakwimu kuwa Tanzania Bara ina majimbo ya uchaguzi 182, kila moja lina wastani wa wakazi takribani 200,000 na Zanzibar majimbo 50 ambalo kila moja lina wastani wa wakazi 20,000.
"Hiyo ni idadi ndogo sana za wakazi. Nchi kama Nigeria yenye wakazi wapatao 140 milioni ina bunge lenye wabunge 360, yaani wastani wa wananchi 400,000 kila jimbo. Nchi kama India yenye wakazi takriban bilioni moja ina wabunge 542 yaani kila jimbo lina wastani wa wakazi karibu 1,700,000.
"Marekani yenye wakazi milioni mia tatu ina wabunge (House of Representatives) 435, yaani wastani wa wakazi zaidi ya 700,000 kila mbunge. Uwakilishi mzuri si wingi wa wawakilishi.
"Kwa hiyo, Tanzania haina budi na uongezaji majimbo ya uchaguzi kila kukicha! Hapana ulazima wowote. La kufanya ni kuwawezesha wabunge kwa kuwapa vitendeakazi vya kutosha."
Kuhusu mfumo wa uwiano, alisema huo ndiyo mfumo rahisi na mwepesi kuandaa kwani hauna bugha ya kugawa nchi katika majimbo, kitu ambacho siku zote ni chenye kusababisha gharama na usumbufu mkubwa.
"Chini ya mfumo huo kila chama kinaanda orodha ya majina kulingana na idadi ya viti vya ubunge. Kulingana na idadi ya kura, kila chama kinapewa asilimia hiyo ya wabunge au viti."
"Baada ya hapo inapotokea nafasi ya kiti cha mbunge au diwani basi chama kinachomoa jina linalofuata kwenye orodha yake na kufilikisha bungeni au kwenye halmashauri ya wilaya manispaa na huyo ndiye, anayekuwa mbunge au diwani mpya."
Alipoulizwa ofisini kwake jana sababu za kuandaa waraka huo, alisema kumekuwa na mambo magumu ambayo maamuzi hayafanyiki, ndiyo maana ameamua kutoa mawazo yake hayo na kuyawasilisha katika ngazi ya chama
0 comments