Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KITAIFA , HABARI ZA LEO - MALECELA AIONYA CCM

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

-ASEMA KAMA INATAKA KUENDELEA KUSHIKA DOLA IWAFUKUZE WATUMUMIWA WA UFISADI
WAZIRI Mkuu mstaafu, John Malecela amekitaka Chama chake cha Mapinduzi (CCM) kuwachukulia hatua za haraka wala rushwa walioko ndani yake kuanzia ngazi ya juu hadi chini kama kinataka kuendelea kushika dola.

Kauli ya Malecela ambaye ni Mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu (CC) ya CCM, inakuja kipindi ambacho mpango mkakati wa chama hicho wa kujivua gamba unaonekana kupigwa kalenda.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi nyumbani kwake Sea…

Mdee ambaye pia ni Mbunge wa Kawe (Chadema), akisoma bajeti mbadala ya upinzani kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa mwaka 2011/12 aliwataja baadhi ya viongozi wa CCM wakiwamo Marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa akiwatuhumu kuhodhi maeneo makubwa ya ardhi mkoani Morogoro huku wakishindwa kuyaendeleza. Hata hivyo, Mkapa anaelezwa kuendeleza shamba lake.

Katika orodha hiyo pia ametajwa Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, Katibu Mkuu wa CCM mstaafu, Philip Mangula, aliyekuwa Naibu wake (Tanzania Bara), Hassan Ngwilizi na Mwenyekiti wa CCM mkoani Mbeya, Nawab Mulla.

Mdee alisema umiliki wa maeneo makubwa ya ardhi unawanyima fursa wananchi wa kawaida kupata maeneo kwa ajili ya shughuli za maendeleo na kuongeza kwamba, vigogo hao kwa kutumia nafasi zao waliwanyang’anya wananchi ardhi hiyo na kujimilikisha wenyewe lakini kwa sehemu kubwa wameshindwa kuyaendeleza.

“Mheshimiwa Spika, matatizo ya ardhi kwa wakubwa kunyang’anya wanyonge imekumba pia Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero ambako mgogoro huu unakumba shamba namba 299 iliyokuwa Narco Ranches lenye ukubwa wa hekta 49,981," alisema na kuongeza:

“Taarifa za kiuchunguzi zinaonyesha kuwa maeneo yaliyokuwa yamepangwa kugawiwa kwa wanavijiji wa Kijiji cha Wami, yamegawiwa wanavijiji wafuatao,’’ alisema na kuanza kuwataja vigogo hao kwa majina mmoja baada ya mwingine.

Akitoa orodha hiyo, Mdee alisema  Mangula anamiliki hekta 2,000, Mwinyi hekta 2,000 na Mkapa hekta 1,000 ambaye hata hivyo, ndiye pekee aliweza kuliendeleza shamba lake.

Katika orodha ya Mdee alimtaja pia  Sumaye kwamba anamiliki hekta 500, Malecela hekta 100 na Ngwilizi ambaye anamiliki hekta 100 huku akisisitiza orodha hiyo ni ndefu.

Mdee alitaka Serikali itoe maelezo kwamba ni vigezo vipi vilitumika kuwagawia ardhi viongozi hao huku wakiwanyima ardhi wananchi wa maeneo husika.

CHANZO: MWANANCHI AGOSTI 22, 2011

MAAFANDE WANASWA

0 comments

Post a Comment