Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KIMATAIFA , HABARI ZA LEO - UTAWALA WA GADDAFI WAANGUKA!

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter Usiku wa kuamkia leo wapiganaji waliokuwa wakipambana na vikosi vya Gadaffi hatimaye wameitwaa Tripoli.  Walibya kwa mamia  waaripotiwa kuingia mitaani kusheherekea ukombozi kutoka kwa utawala wa kidikteta na kikandamizaji. WaLiibya wameonekana wakichoma moto picha za Gaddafi.

Inasemekana wana wa Gaddafi akiwamo Seif Islam ambaye alitarajiwa angemrithi baba yake wako sasa wamekamatwa na wapiganaji hao. Gaddafi mwenyewe hajulikani alipo. Uwanja wa ndege wa Libya kuna ndege mbili ambazo zinadhaniwa Gaddafi angezitumia kuondoka nchini akiwa na familia yake. Gaddafi angekimbilia wapi? Nchi za Zimbabwe na Angola zinatajwa kuwa zingeweza kuwa kimbilio la Gaddafi. Taarifa zaidi zitawajia kadri zitakavyopatikana.

0 comments

Post a Comment