KAULI ya Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, aliyoitoa dhidi ya tuhuma alizotupiwa imezidi kuwasha moto ndani ya CCM baada ya Katibu Mkuu, Yusufu Makamba na Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) Martine Shigela kuendelea kumshutumu, huku baadhi ya wanachama wakimuunga mkono.
Baadhi ya wanachama wa CCM nao wameibuka na kuwashutumu Makamba pamoja na UVCCM kwa kuendeleza malumbano na misimamo ni sumu itakayosababisha mgawanyiko na mfarakano ndani ya chama hicho tawala.
Makamba aliiambia Mwananchi Jumapili kuwa msimamo wa chama ni kwamba Sumaye alikosea kuzungumza nje ya vikoa vya chama na kwamba haina nia ya kumziba mdomo.
Alisema kuwa kitendo cha Waziri Mkuu huyo mstaafu kumshutumu yeye na UVCCM kupitia vyombo vya habari ana lengo la kutaka kuwafunga mdomo wasimkosoe.
"Sisi hatuna mpango wa kumfunga mdomo bali yeye ndiye anataka kutufuanga mdomo," alisema Makamba.
Awali, Makamba na Shigela walisika jana kupitia Redio Uhuru wakitetea misimamo yao ya kumshutumu Sumaye kwa kuzungumza hoja ihusuyo chama nje ya vikao vya chama.
Shutuma zao zimekuja siku moja baada ya Sumaye kukutana na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam na kupinga vikali shutuma dhidi yake akisema hakuvunja kanuni yoyote ndani ya CCM kwa kusema nje ya vikao, kuwa yeye ni kiongozi mstaafu na anategemewa kutoa ushauri wakati wowote inapobidi.
Kauli ya Sumaye iliyozua malumbano hayo ni ile aliyoitoa kwenye mahojiano na waandishi wa habari akisema CCM iache kukaa kimya na badala yake kujibu tuhuma zinazotolewa na chama cha upinzani cha Chadema kupitia maandamano na mikutano ya hadhara sehemu mbalimbali nchini.
Sumaye ambaye alikuwa Waziri Mkuu kwa kipindi cha miaka 10 ya Serikali ya Awamu ya tatu, aliwashutumu Makamba na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi kwa kumuita mtovu wa nidhamu kupitia vyombo vya habari akihoji iweje nao watumie njia hiyo hiyo wanayoikataa badala ya vikao vya chama.
Waziri huo mstaafu alielezea baadhi ya hoja zilizomkera zaidi za UVCCM ambazo alizielezea ni kejeli, matusi na hatari kwa Taifa.
Miongoni mwa hoja hizo ni zile ambazo zilitolewa kwenye maazimio ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa kwamba viongozi wanaosema nje ya vikao watahakikisha wanawapigia kampeni za kuwazuia wasipate uongozi nchini.
Katika kumjibu Sumaye, Makamba jana alisema yeye kama mmoja wa wajumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa, anaunga mkono maazimio yaliyotolewa na UVCCM na kwamba kauli ya Sumaye nje ya vikao vya chama ni kosa.
Katika kuunga mkono maelezo ya Makamba, Shigela alisema iwapo Sumaye aliona kauli za Chadema ni kero na zinapaswa kujibiwa na chama angeweza kuwasiliana na chama hata kupitia tawi analotoka na siyo kusema hadharani.
Wakati viongozi hao wa juu wakionekana kulumbana baadhi ya wanachama wa chama hicho jana walipata fursa ya kutoa maoni yao na wengi kuelekeza makombora yao kwa Makamba na UVCCM kwamba wanakivuruga chama.
Kimaro
Aliyekuwa Mbunge wa Vunjo (CCM), Aloyce Kimaro amesema ni jambo la kusikitisha kuona CCM ikishindwa kutoa tamko lolote juu ya mvutano uliopo kati ya umoja wa vijana wa Chama hicho (UVCCM) na Waziri Mkuu Msfaafu, Frederick Sumaye.
Amesema ukimya huo wa CCM ukiendelea utawafanya wananchi waamini kuwa chama hicho kimepoteza dira kitu ambacho alisema ndio utakuwa mwisho wa chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Akizungumza na Mwananchi Jumapili, Kimaro alisema kinachoitafuna CCM hivi sasa ni makundi yenye fedha yaliyoibuka katika chama hicho.
“Hii sumu ya wenye fedha ndani ya CCM sasa imesambaa mpaka vijijini, CCM isipojivua gamba hili wakati mwaka 2012 ndio uchaguzi wa ndani wa chama kuna uwezekano mkubwa wakapatikana viongozi wa makundi makundi tu,”alisema Kimaro.
Alisema Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete pamoja na Kamati Kuu ya chama ilitizame kwa umakini suala la UVCCM na Sumaye kwa kuwa si vizuri vijana hao kulumbana na viongozi.
Mbunge Nzega
Mbunge wa Nzega (CCM), Dk Hamis Kigwangalla aliiambia Mwananchi Jumapili jana kuwa kimsingi Sumaye ana haki ya kusema ambayo anaona yanafaa kusema na kwamba yeye hafurahishwi na malumbano yanayoendeshwa na umoja wa vijana wa CCM dhidi ya mawaziri wakuu wastaafu.
Alisema huo sio utaratibu wa chama wala haupo katika misingi ya UVCCM. Hata hivyo, alisema pamoja na maelezo yake Sumaye aliteleza aliposema kwamba kiongozi huwekwa madarakani na dola.
Mbunge huyo alisema ingawa anakubaliana na Sumaye kwamba kiongozi huwekwa madarakani na watu lakini, sio dola.
Mjumbe UVCCM
Mjumbe mmoja wa Baraza la UVCCM mwenye Kutoka Nyanda za Juu Kusini ambaye hakutana jina lake litajwe alisema kimsingi alichosema Sumaye hakukosea kwa sababu kama mwanachama ana haki ya kutoa maoni yake kwa njia yoyote kwa kuzingatia kanuni na njia aliyotumia siyo kosa.
Sumaye bado ni kiongozi hata kama amstaafu, ana haki ya kukosoa lolote na kwa kutumia uwanja wowote. Mbona Mwalimu Julius Nyerere akiwa mjumbe wa Kamati ya Kuu mara kadhaa alikuwa akikosoa hadharani na aliwahi kuandika kitabu juu ya viongozi wa Serikali. Kuna tofauti gani kati yao kichama?”
Alisema alisema haoni kosa kwa Sumaye. au Edward Lowassa na mtu mwingine ndani ya chama kukosa na kutoa ushauri wa chama hadharani, isipokuwa anawawasi juu ya kujadali masuala ya chama na nchi kwa misingi kanda.
“Hili la watu kujadili hoja kwa kutoa mifano ya kutoka Kaskazini sikubalini nalo kwa sababu ni hatari kwa taifa, kwani maeneo mengine yatafanya hivyo kwa hiyo itakuwa ni hatari kubwa si kwa chama tu bali kwa mstakabali wa taifa,” alisema mjumbe huyo.
Alisema anachokiona ni kwamba, watu wanasema nje ya vikoa kwa sababu hawapwei nafasi ndani ya chama, au wakisema hawasilizwi, wameshindwa kutumia nafasi yao kutoa duduko lao.
“Kilichopo kwa kuwa chama kinaelekea kwenye Halmashauri Kuuu, Mwenyekiti CCM, Rais Jakaya Kikwete abadili mfumo wa kuendesha vikao kwa kuwapa nafasi na uhuru wajumbe wote kutoa dukuduku lake kama ana nia ya kukimarisha chama,” alisema kada huyo wa UVCCM.
Kada wa CCM, David Msuya mkazi wa Kibaha mkoani Pwani alisema Makamba ameshindwa kukiongozi chama na ndio sababu ya kuibuka kwa migogoro na malumbano ndani ya chama hicho.
Kada huyo aliyefika katika ofisi za gazeti hili jana alisema kitendo cha Makamba na UVCCM kuendeleza malumbano kwenye vyombo vya habari kukiuka taratibu za chama na wanajenga chuki na uhasama miongoni mwa wanachama.
Alisema kwa sasa CCM pamoja na jumuiya zake haukuwa wakati wa kuendeleza malumbano na badala yake ni wakati wa kufikiri wapi wamekiuka hata kusababisha kupoteza majimbo mengi kwenye uchaguzi mkuu uliopita.
Baadhi ya viongozi wenye uzoefu ndani ya chama kuanzia UVCCM waliliambia Mwananchi Jumapili kwamba tatizo kuu linaloiandama CCM kwa sasa ni mgawanyiko unaosukwa na baadhi ya viongozi wenye uelekeo wa kuwa rais 2015.
Kada mwingine naye alionyesha wasiwasi kwamba malumbano na uchochezi unaofanywa na UVCCM kama hautakomeshwa ni rahisi kutokea mpasuko na hata baadhi ya vigogo kujiondoa kwenye chama.
"Ile jana (juzi) wengi tulifikiri Sumaye angetangaza kuwa anajiondoa kwenye chama. Maana mengi yalizungumzwa. Nafikiri wengine walimpigia simu ndiyo maana kwenye maelezo yake alikuwa anasisistiza kwamba yeye ni mwanachama wa CCM na hana mpango wowote wa kukiacha," alisema.
Mmoja wa wabunge wa CCM ambaye naye aliomba jina lake lihifadhiwe alisema UVCCM wanapaswa kuonywa dhidi ya kutoa matamko hovyo hovyo kwa vyombo vya habari.
Alisema kitendo hicho kinaashiria kwamba wanatumiwa na watu jambo ambalo si tu ni hatari kwa chama bali na taiafa kwa sababu mkakati wao wa kuzingatia maslahi unaweza kumuingiza hata dikteta madarakani na wananchi wakaanza kuumia.
Hivi karibuni Baraza Kuu la UVCCM Taifa likitanguliwa na lile la Mkoa wa Pwani, walitoa kauli kali za kuwatisha viongozi wanaokikosoa chama hicho nje ya vikao, wakisema lengo lake ni kuharibu mustakabali wa CCM.
Msimao wa hivi karibuni ni ule uliotolewa Jumapili iliyopita ambapo Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM, Benno Malisa alitoa maazimio ya kikao hicho akisema wamekusudia kuhakikisha kwamba vigogo ambao wamekuwa wakizungumza nje ya utaratibu wa vikao wanatupwa nje ya ulingo wa siasa za chama hicho tawala.
Kauli hiyo aliitoa wakati ambapo katika siku za karibuni baadhi ya makada wa CCM wakiwamo, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe, Edward Lowassa na Sumaye wamekuwa wakinyooshewa vidole na baadhi ya wana CCM wakiwatuhumu kuzungumza mambo ya chama hicho nje ya vikao.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Pwani, Abdallah Ulega aliyasema kuwa wanaozungumza kukisoa chama nje ya vikao wana ajenda yao ya kutafuta urais mwaka 2015.
Hata hivyo, jana alipotakiwa na Mwananchi Jumapili kuzungumzia kauli ya Sumaye ya juzi alisema msimamo wake ni ule ule na kwamba hawezi kuubadilisha kuhusu kiongozi huyo na kwamba anaunga mkono tamko la UVCCM.
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Musoma kupitia Chadema, Alex Malima alisema ya kuwa malumbano baina ya UVCCM na Sumaye ni dalili tosha za anguko la chama tawala na kusisitiza kuwa CCM haina jipya.

0 comments