Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Makamba atumia Biblia kuwalaani Chadema

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Makamba amekilaumu Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kile alichoeleza kuwa kimekaidi amri ya mamlaka halali na kufanya maandamano yaliyoleta vurugu na maafa.


  Akizungumza na gazeti hii jana, Makamba alisema kitendo kilichofanywa na Chadema ni cha kinyama na kinapaswa kulaaniwa na watu wote wanaoitakia mema nchi hii  “Ukisoma Biblia katika kitabu cha Warumi Sura 13, imeandikwa " Itiini Mamlaka inayowazidi nguvu; hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu," alisena Makamba na kuaongeza:  "Sasa mamlaka imesema msiandamane, ninyi mnaandamana.


Nasema hawakufanya vizuri. Sasa tumlaumu nani kama sio Chadema."  Makamba alisema haoni sababu Chadema kuandamana kwa sababu ya suala la Umeya, kwani kama hilo ndio sababu, alipaswa kwenda mahamani kudai haki wanayoeleza kuwa imeporwa na CCM badala ya kufanya maandamano yenye madhara kama hayo. 
"Kama hoja ni umeya, huwezi kudai unayoamini imeporwa kwa maandamano, haki inapatikana mahakamani.

Sasa Mimi (Makamba) nawapa pole walioathirika na maandamano hayo lakini pia nalilia mali za CCM zilizoharibiwa. Gari la katibu wangu wa Mkoa limevunja vioo na ofisi yetu imeharibiwa vibaya," alisema Makamba  mwisho




Comments 





+2#17 mdau kutoka marekani 2011-01-07 11:05
hii nchi yetu inataka kufanywa ya kifalme,bla mtutu tutaendelea hivi hivi kama ako kababu kalivyoongea,kuthamini mali zao kuliko maisha ya watu,we babu naona haela imekaribia kaa mkao wa kula
Quote
+2#16 Emmanuel Shayo 2011-01-07 11:04
Hapa wa kulaumiwa ni serikali, Kwa nn wanaingilia kati wakati damu imeshamwagika na mali kuharibiwa? Wangefanya hivi tangu mwanzo wangeokoa damu za watu. Basi damu hyo iwe juu ya ccm, serikali yake, viongozi wake na familia za viongozi hao
Quote
+2#15 Mteso 2011-01-07 10:56
Wewe Makamba tunakujua wewe ni mkatili sana kwanza tunaomba ukae kimya wewe huna uchungu na watanzania hata kidogo. Sasa hivi tupo kwenye msiba hatuhitaji maneno yako hayo maneno yako nenda kaongelee kule sumbawanga. Tukifuatilia utawala wako na historia yako haifai kuigwa, hiyo mbegu yako ya uongozi inatakiwa ifutwe kabisa. Kwanza uone aibu nasjui kama utazubutu kuwaangali watanzania usuni.
Quote
+2#14 Tulinagwe 2011-01-07 10:47
Huyu Makamba anasema nini, biblia imezungumzia Amani..na yale maandamano ya CHADEMA yalikuwa ya amani isipokuwa hao CCM na serikali yao ndio ilosababisha haya yote mpaka ukatokea uvunjifu wa Amani..na hiyo mahakama vyote ni mali ya ccm na serikali yake, hata siku moja hapa tanzania sijaona haki ya mnyonge yoyote akipelekwa mahakamani inapatikana...nikikumbuka ile kesi ya ZOMBI ndugu zangu walipotez haki zao hivi hivi..CCM MBADILIKE...OTHERWIZE TUNAHITAJI MABADILIKO CHAMA KILICHOPO MADARAKANI KIONDOKE..
Quote
-5#13 MGALAMO 2011-01-07 10:12
mpambanaji haogopi kufa.kama wameamua kupamabana wawe tayari kwa matokeo yote.mnaosema wameporwa umeya. je kwa vipi? maana ninalojua mimi ni kwamba Chadema waligomea uchaguzi wa meya.C.C.M wao wakatumia usemi kama wewe wasusa wenzio twala.sasa nyinyi mlitaka C.C.M wawasubiri hao Chadema mpaka lini? wanaume wa kweli wanapambana kwa hoja katika vikao siyo kususasusa na kukimbilia kupiga kelele nje ya vikao.hayo ndiyo matokeo ya ukaidi na kutoiti dola.kiongozi mzima anaamrisha wafuasi wake wakavamie kituo cha polisi eti wakawatoe watuhumiwa? na bado mnasema polisi wanamakosa.je mlitaka wao wajitetee vipi na mashambulizi ya wananchi? je hao polisi wao hawana roho? lazima tujenge utamaduni wa kukaa pamoja na kushindana kwa hoja siyo kila kukicha mnatoa kauli eti tunawaachia wananchi kuamua wenyewe. yaani mnawajaza jazba halafu mnawaachia waamue wenyewe.na sisi wananchi kwani kuna tatizo gani kama kila mmoja wetu angeelekea katika mkutano wa hadhara kwa njia yake badala ya kuandamana? hivi mnadhani viongozi wa kiafrika watabadilika kwa kuandamana? yaani huko ni kupoteza muda na kujitafutia ulemavu wa viungo ambao baadaye utajuta na watoto wako watakulaumu sana kwa uzembe huo. je hatujifunzi huko pemba? yaani kusoma hatujui hata picha hatuoni? haya wabwana wakubwa wapambanaji. ila kumbukeni lakuambiwa changanya na lako,akili ni nywele kila mtu anazake.sidhani kama Tanzania imefikia mahala watu kuweka rehani uhai wao eti kwa kisingizio cha kuibiwa kura au kuporwa nafasi fulani ya uongozi. kwani hata huyo fulani akishakuwa kiongozi atakuletea pesa ya kula nyumbani pindi utakapopata ulemavu kwa kipigo cha polisi.ndege mjanja ukimbiza bawa lake.
Quote
+3#12 mama bob 2011-01-07 10:08
we makamba acha kutumia biblia vibaya itakulaani,damu za watu zimemwagika shetani sikuhizi anajua sana kuigiza kuwa yuko upande waMungu.
Quote
+3#11 mkereketwasa 2011-01-07 10:05
makamba we mzee tunaomba uzeeke vizuri,kweli unadiriki kufikiria mali za ccm zinazoweza kutafutwa zingine kuliko roho za ndugu zetu ambazo haziwezi kurudi!kumbuka kwamba hizo mali za ccm sio za kwako we2 na watoto wako wala babu yako bali nijasho la watanzania wanaozidi kukandamizwa kila siku.we mzee usilewe na madaraka na kushauri bure uzeeke vizuri usitutie kichefuchefu
Quote
+2#10 albert john 2011-01-07 09:55
haki aipatikani mahakamani kwani mahakama yote ni mali ya kikwete na ccm kama unabisha juzi juzi kikwete kamteuwam jaji mkuu na huyu makamba ameshapita na wakati yeye anafikiri watanzania ni wale wa miaka 70,hata kwenye biblia wameandika amani aipatikani hila kwa ncha ya upanga makamba kaa mkao wa kula na mtafakali samuel dol
Quote
+2#9 john Kundi 2011-01-07 09:42
huyu mzee arudi kwao akalime mkonge,hana anachokifanya hapo dar bali nimaslahi tu ya watu binafsi au tuseme ni EPA tuuu!!
hujui kilichotupata wanachi wa arusha na wala maandiko huyajui waache wanaojua hili waongee.First of all wewe huna taaluma ya huo uongozi wakuvikwa.I hate all ccm pple.....
Quote
+3#8 zombi 2011-01-07 09:28
wewe MAKAMBA NI SHETANI na huna lengo zuri na nchii hii huna Elimu ya biblia tumia msaafu kualalisha mauaji ya Watanzania na sio Biblia.....fisadi mkubwa tunaona jinsi unavyo neemeka na CCM watoto wako wote wako katika position ambazo tukiamua kutrace utakuta hawana qulification za kuwa hapo walipo......TUMIA BUSARA HACHA KUROPOKA INGAWA TUNAJUA KUWA WEWE NI ZUZU.
Quote
+2#7 mwafour 2011-01-07 09:21
We Makamba usilete dharau za kisisiem mpaka kwenye dini, ww ni muislam kilichokufanya utumie biblia ni nini? ccm damu zenu zimejaa uchakachuaji, sasa unajisahau unaleta uchakachuaji mpaka kwenye dini? COMMON SIR USE YOUR BRAIN well, pIA WW NA HAO WENZAKO WOTE KUMBUKENI WOTE MMEUMBWA NA HAMKUJIUMBA MSIJIONE MKO JUU SANA ZAIDI YA ALIEWAUMBA IPO SIKU MTAUMBUKA KAMA ALIVYOUMBUKA FARAU!!!!!!
Quote
+5#6 S.T 2011-01-07 08:44
Makamaba kwa matamshi yako ni wazi unaunga mkono polisi kupiga na kuuwa raia. Hata kama ingekuwa ni kweli kuwa CHADEMA na wananchi walikosea kuandamana bila "kibali" cha polisi bado polisi hao hawakupaswa kutumia nguvu kiasi kikubwa hivyo dhidi ya raia ambao hawakuwa wanaleta vurugu au kuwa na silaha zozote.
MAKAMBA ACHA PROPOGANDA, HII HALI YA POLISI KUUWA RAIA NI YA KUKEMEWA, USILETE SIASA HAPA!!!  @#$@^%@#^%$@ 
Quote
+10#5 Ramadhani 2011-01-07 08:19
Tatizo lako wewe makamba husomi alama za nyakati maana wakati wa zamani ni tofauti na sasa hiki ni kizazi cha utandawazi huwezi kuona unaonewa harafu ukae kimya. Wewe umelazimisha meya Arusha awe wa CCM wakati hana sifa na hakuchaguliwa hapa hata angekuwa mtoto wako asingekubaliwa hebu tumia uongozi wako uwe wa kisasa zaidi then tambua kuna watu wana uelewa kuliko wewe zaidi ya 500%. Hii inchi inaharibiwa na MAKAMBA na vikaneno vyake wa kizamani na anaye sabababisha CCM inagawanyika> MAKAMBA KWA KIFUPI TUNAOMBA UBADILIKE SAWA
Quote
+1#4 tata 2011-01-07 07:54
Ndugu wananchi wenzangu, tusiyumbishwe na wanasiasa wenye chuki zao binafsi: tulime, tufanye biashara,tusome . Kuingia kwa kikwete, silaha au lipumba ikulu hakukusaidii wewe na familia yako kama hujitahidi.MAISHA BARA AU BARA MAISHA HUANZA NA WEWE BINAFSI.
Poleni mliojeruhiwa na mpumzike kwa amani mliokufa.
Kumbukeni Kenya na zenje, wanyonge wameondoka kibaki na mwezake keki na kuku. Kule zenji, sefu kuku kwa mrija na sesem kama kawaida,jamaa ZETU wako ahera!
TUSIDANDANYIKE! TUGANGALIKE!
Quote
+6#3 Bams 2011-01-07 07:42
Huyu Makamba ni mtu hatari kwa Taifa letu. Lowasa alishauri kuwe na mazungumzo, yeye akagoma. Ameng'ang'ania kuwa CHADEMA waende mahakamani. CCM wapore umeya kwa ubabe halafu CHADEMA wakapoteze miaka miwili, mitatu mahakamani. Kweli ukitaka kumjua [NENO BAYA], mwache kwanza aongee ndiyo utapata uhakika. Tunamwomba Makamba asitumie Biblia kuendeleza ubabe, hana elimu ya Biblia, na kila mara ameng'ang'ania kutoa tafsiri potofu. Atumie Msahafu ambao bila shaka anaifahamu vizuri lakini siyo Biblia. kATIKA MAAFA HAYA CHANZO KIKUU NI CCM NA SERIKALI. CCM walpora nafasi ya umeya, serikali kwa kutumia polisi wakaanza kupiga watu ovyo wasio na hatia.
Quote

Tags:

0 comments

Post a Comment