Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Wamiliki wa Dowans Hawa hapa...

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter


Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja  amewataja wamiliki wa Dowans baada ya kupata taarifa kutoka Brela kwa barua yenye kumb. namba MITM/RC/58550/22 ya Januari 5, mwaka huu ambao ni Dowans Holdings S.A, yenye hisa 81 ya Costa Rica na Portek System and Equipment PTE Limited hisa 54 ya Singapore.
Alisema wakurugenzi wa Dowans wa hapa nchini ni Andrew James Tice (Canadian), Gopalakrishnan Balachandran (Indian), Hon Sung Woo (Singapore), Guy Arthur Picard (Canadian), Sulaiman Mohammed Yahya Al Adawi (Oman) na Stanley Munai (Kenyan).
Wakati Ngeleja akitaja majina hayo, wiki moja iliyopita Tanzania Daima ilikwisha kuwataja wanaomiliki kampuni hiyo.
Alisema hakuna sheria inayowataka wawekezaji wakitaka kuanzisha kampuni nchini ni lazima awepo mbia wa ndani, wanaweza kuanzisha wenyewe ikiwa wamefuata taratibu na sheria za nchi.
Alisisitiza kuwa hakuna uhusiano wowote kati ya ulipwaji fidia wa sh bilioni 94 kwa Dowans na TANESCO kupandisha bei za umeme kama ilivyoamriwa na Ewura.
“Ni upotoshaji mkubwa kuhusisha mambo mawili tofauti... migogoro ya Richmond na Dowans ilipelekwa ICC mwaka 2008, sasa kwanini watu wanaunganisha haya? Labda hii inatokana na watu kupenda kuchakachua maneno,” alisema.
Alisema kuwa kuna bidhaa mbalimbali zimekuwa zikiongezeka bei lakini wanashangazwa na hatua ya Ewura kupandisha gharama hiyo kwa asilimia 18.5 na kusababisha baadhi ya makundi kutaka kuandamana wakati ongezeko la bei ya umeme ni suala la kiuchumi na kibiashara kwa shirika hilo.
Alisema wananchi hawana budi kuhakikisha wanasonga mbele na si kuangalia nani aliyeliingizia taifa hasara ili achukuliwe hatua, bali ni kujua hiyo ni sheria na itabaki kuwa historia.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, William Mhando, alisema kuwa mgawo wa umeme bado utaendelea katika maeneo mbalimbali kutokana na kupungua kwa gesi inayosababisha kuwa na upungufu wa megawatts 50 katika grid ya taifa.
Alisema serikali hadi sasa inadaiwa deni la umeme kiasi cha sh bilioni 70, ambapo Waziri Ngeleja aliahidi kufuatilia madeni hayo na kuyakata moja kwa moja kutoka Hazina ili kuyapunguza.

Tags:

0 comments

Post a Comment