Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA LEO - Yanga yaipiga kumbo Simba kileleni

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
TIMU ya Yanga jana imewapiga kumbo kileleni mabingwa wa Tanzania Bara, Simba baada ya kuifunga African Lyon Mabao 3-1 katika
mechi ya Ligi Kuu iliyopigwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na hivyo kuifanya kuongoza kwa tifauti bao moja.

Kwa matokeo hayo Yanga sasa inaongoza ikiwa na pointi 46, sawa na Simba isipokuwa vinara hao wamefungwa mabao saba na kufunga 26  wakati wapinzani wao wamefunga mabao 36 na kufungwa 15 hivyo kuifanya Yanga kuongoza kwa tofauti ya bao moja.

Katika mechi ya jana Yanga iliingia kwa uchu wa kufunga mabao ambapo katika dakika 11, Fred Mbuna aliunganisha kwa kichwa krosi iliyopigwa na Davies Mwape ambayo kipa Ivo Mapunda wa African Lyon aliipangua lakini hata hivyo mpira huo ulitoka nje ya lango.

Yanga ilirudi tena langoni mwa African Lyon ambapo dakika ya 18, Mwape aliachia kombroa kali akiwa nje ya 18 ambalo hata hivyo kipa Mapunda alilipangua na kupata maumivu yaliyomsababishia maumivu na mpira kusimama kwa dakika kadhaa.

Juhudi za Yanga kusaka bao lilizaa matunda dakika ya 32 baada ya Idd Mbaga kufunga baada ya kupokea pasi ya Mwape na kuwazidi ujanja mabeki wa Lyon na kuutumbikiza mpira wavuni.

Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kuingia kwa nguvu na kufanikiwa kupata baoa la pili dakika ya 46 kupitia kwa Mwape ambaye alipiga shuti kali lililomshinda kipa Mapunda ambaye alijaribu kupangua lakini kutokana na kasi ya mpira ya alijikuta akiusindikiza wavuniu.

Dakika ya 61 Yanga ilifunga bao la tatu kupitia kwa Mbaga tena ambaye baada ya kupokea pasi ya Nurdin Bakari alikimbia na mpira na kukutana kipa Mapunda ambaye alimhadaa na kufunga bao kirahisi.

African Lyon ilipata bao lake la kufutia machozi dakika ya 78 baada ya beki Chacha Marwa, kujifunga wakati akiwa katika harakati za kuokoa mpira baada ya Benedicto Ngassa kuachia shuti kali lililokuwa likienda wavuni.

Dakika ya 88, Mbaga alipata dhoruba kali na kuzimia na kutolewa uwanjani kwa machela, baada ya kugongana na Zuberi Makame ambao walikuwa wakiwania mpira wa juu na nafasi yake kuchukuliwa na Razakh Khalfan.

0 comments

Post a Comment