Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Bunge la 10 lina mambo yake...haya hapa

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
MBUNGE WA VUNJO MH AUGUSTINE MREMA


Ni Mbunge wa Jimbo la Vunjo, Mhe. Augustino Mrema. Alinaswa na Mlalanje akiwa ametulia nje ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma hivi karibuni.

Haikuweza kufahamika alichokuwa akifanya licha ya kuonekana akiwa ameishika simu yake kama mtu anayetuma sms au kutaka kupiga.

MBUNGE WA ROMBO MH. JOSEPH SELASINI
Jioni ya Jumanne iliyopita ndiyo Mbunge wa Rombo (CHADEMA), Joseph Selasini aliwasili Dodoma tayari kwa ajili ya kufanya usajili bungeni lakini kilichomvuta mwandishi wa makala haya ni mkono wake wa kulia ambao ni mbovu.

Mwandishi wetu alikutana na Selasini katika Pub inayoitwa Wende, iliyopo eneo la Area C ambapo alisema kuwa mkono wake wa kulia ulivunjika mara tatu alipokuwa kwenye shughuli za kampeni.

“Kidogo nife, ile ajali hata siielewi, watu wote walipona tena hata kuchunika kidogo lakini mimi peke yangu ndiyo nikawa hoi,” alisema Selasini, mwanasiasa wa siku nyingi aliyevuma miaka ya nyuma akiwa NCCR-Mageuzi.

Akiwa na mkono uliozungushiwa bandeji ngumu (muhogo), Selasini aliyemshinda mwanasiasa mkongwe nchini, Basil Pesambili Mramba alisema kuwa ushindi wake ni sawa na mende kuangusha kabati.

“Nilipokuwa nagombea kila mtu alisema mimi ni mende nashindana kuangusha kabati, lakini niliwaambia kwamba mende wa kwetu Rombo wana nguvu sana, kwahiyo wanaangusha kabati,” alisema Selasini.

Kuhusu ujio wake ndani ya bunge jipya, Selasini alisema: “Ni wakati wa kuwatumikia wananchi, ndugu zangu wa Rombo wameniamini, kwahiyo nitafanya zaidi ya matarajio yao.”

Hussein Mwinyi na mkewe, Mariam Mwinyi.

Aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Usalama katika muundo wa serikali iliyopita, Hussein Mwinyi na mkewe, Mariam Mwinyi muda wa jioni wakiwa Dodoma huwa ‘bize’ barabarani wakifanya mazoezi.

Hamis Kagasheki.


Ukimuona barabarani inatosha kukupa picha kwamba mwili wake umejitosheleza, afya yake siyo ya wasiwasi, kumbe siri ya mafanikio yake ni hii.

Mbunge wa Bukoba Mjini (CCM) na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani katika serikali iliyopita, Balozi Hamis Kagasheki ni hodari wa kufanya mazoezi na kila siku jioni hupatikana barabarani labda awe ametingwa na shughuli za bunge.
Tags:

0 comments

Post a Comment