Wapiga kura na wageni waalikwa wakiwa ndio wamewasili Mjengoni tayari kuanza shughuli ya kuwachagua viongozi wao kwa mwaka 2010/2011. Wa Kwanza (suti Nyeusi ni Juvenile Mwambi)
Tume ya Uchaguzi iliyoongozwa na Bw. Livingston Swilla (a.k.a Mbunge) ikiwa tayari kabisa kuanza zoezi hilo. Bw. Mbunge ni mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi tangia mwaka 2007.
Kazi imeanza rasmi kwa wimbo wa Taifa. Hapa wakiimba wimbo wa Taifa
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Bw. Swilla akiwa tayari na karatasi za kupigia kura ready kuanza zoezi zima
Aliyekuwa Mwenyekiti wa serikali hiyo ya wanafunzi Bw. Isaac Isanzu akiachia ngazi
Mgombea wa nafasi ya mshika fedha akinadi sera zake. Hata hivyo alizidiwa nguvu na mpinzani wake ambaye alichaguliwa kushika nafasi hiyo
Mgombea nafasi ya mshika fedha akinadi sera zake. Binti huyo alishinda kwa kishindo kilichomzidi mpinzani wake ka kura kibao.
Wadau na wapiga kura wakisubiria kwa hamu matokeo ya uchaguzi huo
Mwenyekiti mteule Bw. Kasimu Kolowa. Bw. Kolowa ameshika nafasi hiyo kwa kupata ushindi wa kishindo kilichowazidi wapinzani wake watano. Kwa historia Bw. Kolowa alizidiwa kwa kura tano tuu katika uchaguzi uliofanyika mwaka jana .
Mgombea nafasi ya mshika Fedha msaidizi na Mtangazaji wa zamani wa Radio Tanzania (anayezungumza) akinadi sera zake. Hata hivyo alizidiwa nguvu na mpinzani wake ambaye kwa kishindo alinyakua nafasi hiyo.
Bi. Odilia Kasiga aliyeteuliwa kusika nafasi hiyo baada ya kumbwaga mpinzani wake kwa kishindo kikubwa.
Mwenyekiti mteule akiwa na wadau mbalimbali na wazee wa mji
Mh. Balozi wa Tanzania Mh. Capt. Mstaafu Jaka Mwambi akiongea na wapiga kura mara baada ya uchaguzi huo.
Katibu anayemaliza muda wake akikabidhi risala kwa Mh. Balozi
Picha ya pamoja mara baada ya Uchaguzi
sasa wewe mtangazaji wa redio Tz, huoni kama umeezeekaaaaaaaaaaa??? waachie vijana , umri wako mkubwa mama!! unajiabisha bure na CV za kubumba, kwani rekodi zako tunazo toka umefika . Tatizo una ruka vihunzi kama kuku wa kienyeji! chumba kwa chumba, LUMUMBA YOTE GUMZO !Duu pole.
Man KIGO! Hongera Man...! Manake nilidhani masihala, ila mdogo wangu kuna kitu naomba nikushauri, KWA HESHIMA ZOTE NAOMBA UMTEU BI JANETH SHEM AWE NDO MSHAURI WAKO MKUU WA MASWALA MAGUMU YA JAMII NA SERIKALI! HUYU DADA ANAONEKANA ANAUADILIFU MKUBWA NA MAADILI . HANA MAKUU.!! UKIWA NAE KARIBU UTAFANIKIWA SANA katika Uongozi wako. WASIWASI WANGU MI KWAMBA KAMA HUNA MSHAURI MAKINI, YATAKUKUTA KAMA YALIVYOWAKUTA!! hatutaki kukupoteza, manake kauli za Serikali Jana, zilikuwa na Utata Mno. Kauli nzito nzito!! Ukimteu huyo Dada Utajiamini zaidi! Manake Makamu mwenyekiti UTATA MTUPU!! :)))))