Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Lowassa kung'olewa

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter MBUNGE wa Monduli, Waziri Mkuu aliyejizulu, Edward Lowassa, anakabiliwa na wakati mgumu wa kuteuliwa kutetea kiti cha ubunge katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 31, Tanzania Daima Jumapili limebaini.
Lowassa ambaye alijiuzulu uwaziri mkuu Februari 7, 2008 kutokana na kuhusishwa na kashfa ya kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond, anakabiliwa na upinzani kutoka kwa makada waliojitokeza kuwania ubunge wa jimbo la Monduli kwa tiketi ya CCM.

Lowassa ameshikilia jimbo hilo kwa miaka 20. Mchakato wa kura za maoni ndiyo utakaotoa jibu la mtu atakayeteuliwa na CCM kugombea ubunge wa jimbo hilo.

Baadhi ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameliambia Tanzania Daima Jumapili kuwa hatua ya watu wengi kujitokeza kupambana na Lowassa inachangiwa zaidi na kuwapo kwa makundi yanayokinzana ndani ya chama hicho kikongwe.

Hali hiyo inadhihirisha wazi kuwa hakuna mbunge katika uchaguzi mkuu ujao ndani ya mkoa wa Arusha ambaye atatetea jimbo lake kirahisi kama ilivyozoeleka katika chaguzi nyngi zilizopita kwa baadhi ya majimbo wagombea kupita bila kupingwa.

Katika jimbo la Monduli, kwa muongo mmoja sasa, Lowassa amekuwa akipita bila kuwa na upinzani mkubwa hususani ndani ya chama chake.

Mpaka sasa makada waliokwishajitokeza kukabiliana na Lowasa ni pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) mkoa wa Arusha Danieli Ole Porokwa.

Kada mwingine wa chama hicho kikongwe nchini aliyetangaza nia yake ya kugombea jimbo hilo ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Dk. Ibrahimu Toure, anayeonekana kuwa na ushawishi mkubwa.

Porokwa ndiye anatarajiwa kutoa upinzani mkubwa kwa Lowassa kutokana na historia ya wanasiasa hao tangu katika kinyang'anyiro cha kuwania urais mwaka 2005 ambapo Porokwa alikuwa akimuunga mkono John Malecela ambaye alitangaza kuwania urais huku Lowassa akimuunga mkono Rais Kikwete aliyeibuka mshindi.
Tags:

0 comments

Post a Comment