Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Mswada Uganda wa kunyoga mashoga warekebishwa

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Mbunge wa Uganda aliyependekeza kuwepo kwa hukumu ya kifo kwa baadhi ya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja amesema yuko tayari kubadilisha rasimu ya mswada.
Katika mahojiano na gazeti la Daily Monitor, David Bahati amesema alizungumza na baraza la mawaziri kuhusu mswada huo na alikuwa tayari kurekebisha baadhi ya vipengele.
Mapema wiki hii baraza la mawaziri liliunda kamati kujadili mapendekezo ya Bw Bahati.
Mapendekezo hayo yamesababisha ukosoaji kutoka maeneo mbalimbali duniani, huku nchi nyingine za kimagahribi zikitishia kusitisha utoaji wa misaada iwapo mswada huo utakuwa sheria.
Wiki iliyopita Rais Yoweri Museveni alikiambia chama chake kuwa hilo kwa sasa ni suala linalohusu sera za kigeni.
Tags:

0 comments

Post a Comment