Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Kwaheri Twanga Pepeta. waamia Extra Bongo ya Ally Choki

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
BENDI ya muziki wa dansi nchini, Twanga Pepeta leo imepata pigo jingine tena baada ya kuondokewa na wanamuziki wake wengine watano kujiunga na bendi ya Extra Bongo inayomilikiwa na Ally Choki Rwambo (Mzee wa Farasi).

Utambulisho wa wanamuziki hao wapya kwa waandishi wa habari umefanyika leo katika ukumbi wa Meeda uliopo Sinza Mori jijini Dar.

Akizungumza kabla ya kuwatambulisha wanamuziki hao, Choki amesema sasa ni zamu ya bendi yake kulikamata jiji, hivyo aliwaomba mashabiki wake wakae tayari kuipokea Extra Bongo mpya.

Wanamuziki hao ni:  Issack Buriani  ‘Super Danger’, Saulo John ‘Ferguson’, Rogert Hegga ‘Caterpilar’, Otilia Boniface ‘Kandoro’ na Hassan Musa ‘Nyamwela’.

Wanamuziki wengine kutoka nje ya Twanga Pepeta ni Oseah pamoja na George Kanuti waliokuwa wakifanya shughuli za muziki nchini Muscat.




Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Choki, aliyenyoosha mkono akimtambulisha mpiga gitaa la besi (Oseah) aliyevaa kofia na miwani.
‘Ferguson’ akitafakari jambo.
Ally Choki akimtambulisha Otilia Boniface ‘Kandoro’.
Mzee wa Kisigino  (Ferguson) akiwa katika pozi.
Tags:

0 comments

Post a Comment