Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Hoja binafsi ya mwakilishi yaitisha kikao CCM Zanzibar

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
CHAMA tawala, CCM jana kiliwaita wajumbe wake kwenye Baraza la Wawakilishi kujadili hoja inayozidi kuongezeka nguvu ya kutaka rais wa sasa wa visiwani hapa, Amani Abeid Karume aongezewe muda ili akamilishe kazi inayoelezwa kuwa ni ya kumaliza siasa za chuki.

Kikao hicho kilifanyika kwenye ofisi za makao makuu ya chama hicho yaliyo Kisiwandui baada ya Abubakar Khamis Bakari, mbunge wa chama kikuu cha upinzani Zanzibar, CUF, kuwasilisha hoja binafsi ya kutaka Karume aongezewe muda.

Kwa mujibu wa habari za ndani ya kikao hicho, ajenda kuu ilikuwa ni kuwapa habari wajumbe hao juu ya hoja binafsi itakayowasilishwa na kiongozi wa kambi ya upinzani kwenye Baraza la Wawakilishi na kutenguliwa kwa vipengele vya katiba ili Rais Karume aongezewe muda, jambo ambalo baadhi ya viongozi wameonyesha kulipinga hadharani.

Wananchi wa kawaida wamekuwa wakivumisha habari kwamba hoja binafsi imeshawasilishwa na serikali ya umoja wa kitaifa itaundwa hivi karibuni huku wengine wakifuatilia kila mara habari za mwenendo wa suala hilo.

Wakati hayo yakiendelea, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wanasuburi kwa hamu kubwa hoja hiyo binafsi isomwe barazani wiki ijayo.

Hayo yalibainika katika shughuli za baraza zinazoendelea baada ya baadhi ya wajumbe kuonekana kutokuwa na hamu ya kuchangia na kujadili miswaada inayowasilishwa katika kikao hicho.

Juzi uliwasilishwa mswaada wa Sheria ya Utangazaji na mswaada wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka lakini wajube wamekuwa wakichangia kwa muda mfupi sana kinyume na kawaida yao.

"Tunasubiri kujadili mambo mawili zaidi, hasa hoja binafsi kuhusu serikali ya umoja na tunasubiri kujadili Sera ya Nishati kwa sababu hayo ndio mambo makubwa katika kikao hiki si wenyewe waandishi mnaona mambo yanavyokwenda," alisema mwakilishi mmoja wa CCM.

"Siku hizi huko nje kila mtu anazungumzia mambo ya mseto basi na sisi ni binaadam eti, ndio tunasubiri."

Hata hivyo mwakilishi huyo hakuwa tayari kueleza kwamba anaunga mkono au anapinga, lakini alisema kwa kuwa hoja hiyo itawasilishwa barazani hamna budi kusubiri jinsi wawakilishi watakavyochangia.

"Mimi nitamuona mtu wa ajabu sana iwapo kuna mjumbe atapinga suala la kuahirishwa kwa uchaguzi kwa sababu hakuna hata mtu mmoja wa visiwa hivi vya Unguja na Pemba ambaye hafahamu suala la maafa yanayotokana na uchaguzi na hakuna asiyejua kuwa zanzibar chaguzi zetu zina matatizo makubwa na hili si CUF peke yao wanaoathirika, hata sisi CCM," alisema mmoja wa wajumbe.
Tags:

0 comments

Post a Comment