Bunge la Angola limepitisha kuwepo kwa katiba mpya itakayofuta uchaguzi wa moja kwa moja wa nafasi ya Rais.
Kiongozi wa nchi sasa atateuliwa na chama chenye idadi kubwa ya wawakilishi bungeni.
Chama kikuu cha upinzani, Unita, kimegomea kura hiyo, kikiishutumu serikali kwa kujaribu kuvuruga demokrasia.
Rais Jose Eduardo dos Santos amekuwa madarakani kwa zaidi ya miongo mitatu na uchaguzi mwengine hautarajiwi kufanyika hadi mwaka 2012.
Nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta bado inajaribu kurejesha hali ya utulivu na usalama baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kumalizika mwaka 2002.
Shirika la habari la AFP limesema mabadiliko hayo yamepitishwa na wabunge 186 miongoni mwa 220 yaliyovutia hamasa huku wakishangilia kwa nguvu "Angola, Angola!"
0 comments