Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Msekwa apewa miezi mitatu alipe deni la mtoto wake

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imempa miezi mitatu, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa awe amemaliza kulipa deni la Sh 7,072,000 serikalini zikiwa ni sehemu ya fedha zilizolipwa kwa ajili ya matibabu ya mwanae Julias.

Julias Msekwa alipatwa na hali ya ugonjwa wakati akiwa safarini katika treni kutoka nchini Uingereza jijini London kwenda Paris Ufaransa kikazi, wakati huo alikuwa ni mafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza.

Uamuzi huo wa PAC umetolewa jana baada ya majumuisho ya kikao cha kamati hiyo kilichokutana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika ofisi ndogo ya Bunge, Dar es Salaam

Katika uamuzi wake huo, PAC ilisema Msekwa anapaswa kulipa fedha hizo ndani ya kipindi hicho kutokana na deni hilo kuwa la muda mrefu tangu mwaka 2003.

Lakini, mwenyewe Msekwa alikiri akisema,: "Ni kweli nina deni la kama Sh 7 milioni lililotokana na mwanagu Julias ambaye kwa wakati huo alikuwa ni mfanyakzi wa ubalozi wa Tanzania London, Uingereza kuugua gafla katika treni wakati akiwa safarini kikazi kutoka London kwenda Paris."

Msekwa alikopeshwa na wizara hiyo kiasi cha Sh 10,072,000 kwa ajili ya matibabu ya mtoto wake huyo, ambaye alianguka akiwa ndani ya treni na kubainika ni raia wa Tanzania baada ya kuangaliwa hati yake ya kusafiria.

Msekwa jana alilithibitishia Mwananchi kudaiwa deni hilo, lakini akadai kuwa kuchelewa kuzilipa fedha hizo ni kutokana na kuchelewa kupata hati ya malipo(invoice).

Awali, kuliibuka utata kuhusu jina la kigogo huyo baada ya maafisa wa wizara hiyo kukataa kumtaja jina wakisema mhusika (mdaiwa) ni kigogo ndani ya chama alikuwa hana ajira lakini sasa hivi ana ajira.

Hatua hiyo, iligawa wajumbe ambao baadhi walitaka atajwe, lakini wengine walipinga kutokana na kuogopa waandishi wa habari.

Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema) Lucy Owenya, alihoji hofu kwa waandishi wakati kilichokuwa kikijadiliwa ni fedha za umma, lakini wengine kama kina Issa Kassim Issa (Mpendae), alijaribu kujenga hoja ya kumsitiri mdaiwa kwa madai hata Mungu husitiri wanaositiri wenzao.

Baadaye, waandishi wenyewe waliamua kutoka, lakini mwenyekiti John Cheyo ambaye awali hakuwepo, aliporejea aliwasihi wanahabari hao wasiondoke.

Lakini, mwenyewe Msekwa alikiri akisema,: "Ni kweli nina deni la kama Sh 7 milioni lililotokana na mwanagu Julias ambaye kwa wakati huo alikuwa ni mfanyakzi wa ubalozi wa Tanzania London Uingereza kuugua gafla katika treni wakati akiwa safarini kikazi kutoka London kwenda Paris."

"Nilichelewa kulilipa deni hilo kutokana na kuchelewa kupata Invoice(stakabali ya maelezo ya malipo), lakini tayari nimekwishaanza kulipa na tayari nimekwisha lipa Sh 3 milioni."

Makamu mwenyekiti huyo wa CCM, alifafanua kwamba, 'stakabadhi hiyo hiyo aliipata mwaka jana na amejiwekea kulipa Sh 1milioni kila atakapo pata uwezo.

Aliongeza kwamba, hata katika fomu yake aliyojaza kwa ajili ya kuonyesha mali na madeni aliyonayo ametaja kuwa na deni hilo.

Baadaye, Cheyo alifafanua, "Jamani hizi fedha hakuziiba, ila alikopeshwa kama anavyoweza kukopeshwa Mtanzania mwingine, hivyo asifikirike vibaya ila tatizo ni kuwa amechelewa kulilipa hili deni," alifafanua Cheyo.

Katika hatua nyingine, Kamati hiyo imeutuhumu Ubalozi wa Tanzania nchini Japan kwa kuwalipisha Watanzania wanaolewa au kuoa nchini humo fedha kinyume cha utaratibu.

Tuhumu hizo zilitolewa na mbunge wa Mpendae, Issa Kassim ambaye ni mjumbe wa kamati hiyo.

"Ninao ushahidi kuhusu hilo na mkitaka nitautoa na mbaya zaidi mnawalipisha kwa dola 200 za Marekani, lakini katika risiti za malipo mnaandika kwa Sh (fedha za kitanzania)," alisema Kassim.

Kutoka na tuhuma hizo katibu mkuu wa wizara hiyo, Sasu Salula amelazimika kumuagiza mkaguzi wa mahesabu wa wizara hiyo nchini Japan.
Tags:

0 comments

Post a Comment