Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Serikali yaitupia mahakama mgombea binafsi

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
SERIKALI imesema hatima ya mgombea binafsi kushiriki katika chaguzi mbalimbali nchini iko mikononi mwa Mahakama ya Rufaa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Philip Marmo alisema hayo jana wakati wa kukusanya maoni ya wadau juu ya sheria za uchaguzi katika zoezi linalosimamiwa na Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ya Bunge.
Akijibu hoja zilizotolewa na mwakilishi wa Chama cha Wananchi (CUF), Joram Bashange juu ya kuruhusiwa kwa mgombea binafsi katika uchaguzi mkuu, kiongozi huyo alisema suala hilo liko kimchakato zaidi.
Marmo akitoa ufafanuzi wake kwa wanahabari nje ya Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, alisema tayari Mwanasheria Mkuu wa Serikali, amekwishaagiza mahakama iangalie kama ina uwezo wa kuibadilisha sheria inayotaka wabunge kuwa ndani ya chama.
“Tatizo hatuwezi kuiga wengine. India na Ujerumani kwao hawataki kabisa suala hili, inategemea na mazingitra ya kwao yako vipi, lakini mwanasheria mkuu amekwishaiambia mahakama kama ina uwezo wa kubadilisha sheria hiyo,” alisema Marmo.
Katika hatua nyingine, mwanasheria kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Laetitia Petro alisema katika marekebisho ya sheria hizo, suala la mgombea wa chama fulani kupita bila kupingwa ni kuwakosesha wananchi haki zao.
Mwanasheria huyo alisema ni bora uchaguzi ukahairishwa hata kama serikali itaingia gharama ili kuepuka kumpata mgombea ambaye watu hawamtaki.
Tags:

0 comments

Post a Comment