JERUSALEM
You Are Here: Home - - Mazungumzo ya Amani Mashariki ya Kati yako hatarini
IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya, Cathereine Ashton amemaliza ziara yake ya siku moja nchini Israel na katika maeneo ya mamlaka ya Palestina, huku akizitaka pande zote mbili ziendelee na mazungumzo ya amani.Akizungumza na waandishi habari mjini Jerusalem, Ashton alisema mazungumzo yake na viongozi wa Israel pamoja na Wapalestina yalikuwa mazuri na yakutia moyo. Ashton alikuweko Jerusalem na Ramallah kujaribu kuyaokoa mazungumzo ya ana kwa ana kati ya pande hizo mbili yaliyoanza wiki nne zilizopita. Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas alisema mazungumzo hayo hayawezi kuendelea iwapo Israel itaendelea na ujenzi wa makaazi ya walowezi katika Ukingo wa Magharibi, eneo ambalo Wapalestina wana matumaini yatakuwa sehemu ya taifa lao huru. Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesisitiza nia ya kuendeleza mazungumzo hayo, lakini amekataa kusalim amri kwa shinikizo la Jumuiya ya Kimataifa kurefusha muda wa kusitisha ujenzi wa makaazi hayo ya Wayahudi uliomalizika wiki iliopita.
0 comments