Taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo la nchini Marekani, Dk. William Morris, iliyotumwa kwa Mengi jijini Dar es Salaam na Tanzania Daima kupata nakala yake, ilisema Mengi ni miongoni mwa watu hao ambao wameteuliwa na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) zaidi ya 10,000 yaliyosajiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN).
Mbali na Mengi, taarifa hiyo iliwataja watu wengine maarufu duniani walioteuliwa kuwania tuzo hiyo na nchi zao kwenye mabano kuwa ni pamoja na aliyekuwa Makamu wa Rais wa zamani wa Marekani, Al Gore (Marekani), Sir Roger Moore (Uingereza) na mchezaji maarufu wa soka nchini Liberia, George Wear. Kwa sasa Wear ambaye alijipatia umaarufu mkubwa duniani kisoka ni balozi wa masuala ya amani Barani Afrika.
Moja ya vigezo vinavyotumika kuteuliwa kuingia kwenye tuzo hiyo ni pamoja na kuangalia ushiriki wa mhusika jinsi alivyojitoa bila kuchoka katika kusaidia malengo ya Mpango wa Millennium katika kuondoa umaskini, kuboresha afya za jamii katika nchi husika.
Mshindi wa tuzo ambayo ni moja ya tuzo kubwa na za heshima zinazotambulika duniani, anatarajiwa kutangazwa katika hafla ya harambee ya kuchangia mfuko maalum, itakayofanyika Novemba katika ofisi za makao makuu ya Umoja wa Mataifa, mjini New York, Marekani.
0 comments