Afrika inaendelea kiuchumi lakini maendeleo ya kidemokrasia yamebadilika, takwimu za mwaka huu zinaonyesha.
Takwimu za wakfu wa Mo Ibrahim za utawala bora wa Tanzania zimeorodhesha nchi 53 za Afrika kulingana na alama 88, kuhusiana na masuala ya rushwa hadi elimu.
Mauritius iko nafasi ya juu huku Somalia ikiwa chini kabisa.
Takwimu hizo zinaonyesha kote barani Afrika, masuala ya kiuchumi na afya yanarejeshwa nyuma na kuporomoka kwa haki za kisiasa, usalama na utawala wa sheria.
Takwimu hizo ambazo zimechapishwa tangu mwaka 2007, zinatoa alama kuannia sifuri hado 100.
Inadhaminiwa na tajiri wa masuala ya mawasiliano wa Sudan Mo Ibrahim.
Bw Ibrahim alisema katika taarifa yake, " Wakati raia wengi wa Afrika wanaanza kuwa na afya njema na fursa nyingi za kiuchumi kuliko miaka mitano iliyopita, si wengi wanapata nafasi ya kushiriki kwenye uchaguzi."
Katika ripoti ya mwaka huu, wastani wa alama zilizopatikana ni 49- ambazo hazijabadilika sana ukilinganisha na miaka ya awali.
Mauritius ina alama 82, Seychelles 75 na Botswana 74 kwa jumla ya alama zote, huku Somalia yenye alama 8, Chad 31 na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ikiwa na alama 32, zote zikiwa na alama ya chini.
Angola, Liberia na Togo wameimarika sana kwenye alama zao, huku Eritrea na Madagascar zikiporomoka sana.
Vielelezo vimegawanywa katika alama ya makundi manne. Katika makundi mawili, Fursa ya Uchumi Endelevu na Maendeleo ya Binadamu, nchi nyingi zilionekana kufanya vizuri, na hakuna nchi iliyoporomoka katika vigezo hivyo.
Lakini katika makundi mengine mawili- Usalama na Sheria, na Ushiriki na Haki za Binadamu- taarifa kidogo iko tofauti.
'Mfadhaiko'
Kwa suala la uchumi, mengi yamefanyika, huku mataifa 41 miongoni mwa 53 yakionyesha kuimarika.
Hakika, Bw Ibrahim alisema Afrika inakua mara nne zaidi ya Ulaya, ikisaidiwa na kuongezeka kwa kasi ya matumizi ya simu za mkononi na malighafi za viwandani.
Mhariri wa BBC wa masuala ya Afrika Martin Plaut alisema, hizi ni takwimu za kuhuzunisha.
Alisema nchi zilizopata alama chache, kama vile Somalia, Sudan na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wote bado wanakabiliwa na uasi pamoja na vita vya wenyewe kwa wenyewe- matatizo ambayo Afrika ilitakiwa iyatatue zamani.
0 comments