Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA MICHEZO - Arsenal yaongoza Ligi kuu ya Uingereza baada ya kuibamiza Bolton 4 - 2

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Arsenal iko juu katika msimamo wa ligi ya premia ya England baada ya kupata ushindi wa magoli manne dhidi ya mawili ya Bolton.
Gary Cahill aliipatia Bolton bao la kwanza katika dakika ya saba na Matthew Taylor akaongeza la pili kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 28.
Lakini Arsenal wakajitahidi na Tomas Rosicky akaipatia timu yake bao la kwanza katika dakika ya 43 kabla ya Cesc Fabregas kusawazisha kwa kufunga goli la pili dakika saba baada ya kuanza kwa kipindi cha pili.
Bao la tatu lilifungwa na Thomas Vermaelen naye Andrey Arshavin akakamilisha idadi ya magoli manne.
Ilikuwa usiku mzuri kwa kocha Arsene Wenger, ambaye timu yake ilikuwa imefungwa magoli mawili baada ya dakika 28 na walihitaji ushindi wa magoli mawili zaidi ili waweze kuwa juu ya msimamo wa ligi.

0 comments

Post a Comment