Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KISIASA , HABARI ZA LEO - Uchaguzi wa Tawi la CCM Russia wanukia

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya tawi la CCM Moscow-URUSI ilimaliza kikao chake cha masaa 3, jioni ya tarehe 23 /02/2012 Mjini Moscow, chini ya Uenyekiti wa Mwenyekiti wa Tawi, Dr Alfred Kamuzora ambapo 80% ya wajumbe wote wa kamati ya Siasa walihudhuria . Kikao hicho cha dharula kiliitishwa kwa Ajenda moja kuu ya utekelezaji wa Maagizo ya HALMASHAURI KUU TAIFA ya CCM “NEC” kuhusu Uchaguzi wa viongozi wa chama cha mapinduzi katika ngazi mbalimbali mwaka 2012,
Kwa Muhtasari huo, Pamoja na mambo mengine Kamati ya siasa ya tawi  imeagiza utekelezaji wa mambo yafuatayo, yanayohusu;
1.UCHAGUZI WA VIONGOZI WA JUMUIYA WANAWAKE TAWI LA CCM MOSCOW.
Kwa kuwa Jumuiya ya wanawake tawi ilifanya Uchaguzi , mwezi May 2011 ,na kwa kuwa Uchaguzi huo ulizingatia vigezo vya Uchaguzi kwa wagombea na wanachama wa Jumuiya husika na kuufanya uchaguzi huo kuwa Huru na Haki na Viongozi wapya kuchaguliwa, Kamati ya siasa ya tawi imeridhia KUTOFANYIKA UCHAGUZI MWINGINE NDANI YA JUMUIYA YA WANAWAKE TAWI LA CCM MOSCOW- 2012.
Aidha Kamati ya siasa ya tawi imewataka viongozi wote wapya wa UWT waliochaguliwa , kujaze form maalumu  iliyotolewa na NEC ili kukamilisha mchakato huo na kuweka kumbukumbu sahihi ya kiofisi ya viongozi wa chama cha mapinduzi –Makao Makuu , Dodoma Tanzania.
2.UCHAGUZI WA VIONGOZI WA JUMUIYA YA VIJANA YA TAWI (UVCCM)
Kamati ya siasa ya tawi, imeiagiza Jumuiya ya Vijana ya tawi chini ya mwenyekiti wake Bw. Mahomoud Mbarouk , Kuhakikisha  Uchaguzi wa Viongozi wapya wa Jumuiya  hiyo uwe UMETEKELEZWA ifikapo tarehe 25/3/2012. Aidha kamati ya Siasa imeanisha nafasi za kugombea Uongozi ndani ya Jumuiya hiyo ni kama ifuatavyo:- 
i) Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana ,Tawi la CCM Moscow.
ii) Katibu wa Jumuiya ya Vijana ,Tawi la CCM Moscow.
iii) Katibu wa Fedha na Uchumi wa Jumuiya ya Vijana , Tawi la CCM Moscow.
iv) Katibu wa Uhamasishaji wa Jumuiya ya Vijana , Tawi la CCM Moscow.
v) Wajumbe 15 wa Baraza la Vijana la Jumuiya ya Vijana wa CCM Moscow.
Form za Kugombea Nafasi tajwa hizo za Uongozi wa UVCCM ,zinapatikana kwa Katibu wa Jumuiya ya Vijana wa tawi Bw.OCTAVIAN NYALALI.

3. UCHAGUZI MKUU WA VIONGOZI, NGAZI YA TAWI LA CCM MOSCOW- 2012.
Kwa kuzingatia maagizo na malekezo ya kalenda ya Uchaguzi wa Viongozi wa CCM ngazi ya Matawi iliopitishwa  na NEC , kilele cha chaguzi hizo ni tarehe 28/4/2012. Kwa zingatio la kalenda hiyo, kamati ya siasa ya tawi imepanga Utaratibu stahiki  kuhakikisha zoezi hilo la Uchaguzi linafanyika katika mazingira mapana ya huru na haki  na kukuza Demokrasia ndani ya chama cha mapinduzi kama ifuatavyo:
Tarehe 15-22/4/2012:- Zoezi la Uchukuaji na Urejeshwaji wa FOM ZA WAGOMBEA kwa ngazi mbalimbali za Uongozi wa CCM, Tawi la Moscow Urusi.
Tarehe 25/4/2012:- Taarifa kwa wanachama wa CCM tawi kuhusu MAJINA ya Wanachama wa CCM, wanaomba ridhaa ya kuongoza TAWI LA CCM MOSCOW.
Tarehe 28/4/2012:- Uchaguzi Mkuu wa Viongozi NGAZI YA TAWI LA CCM MOSCOW.
Kamati ya siasa ya Tawi, imeanisha nafasi za Kugombea Uongozi ngazi ya Tawi kama ifuatavyo:
i) Mwenyekiti wa Tawi la CCM Moscow.
ii) Katibu wa Tawi la CCM Moscow.
iii) Katibu wa Fedha na  Uchumi  wa Tawi la CCM Moscow
iv) Katibu wa Sera na Uenezi wa Tawi la CCM Moscow
v) Wajumbe 5 wa kamati ya Siasa ya Tawi.
vi) Wajumbe 12 wa  Halmashauri kuu ya Tawi la CCM Moscow.
Form za Kugombea nafasi hizo tajwa zinapatika toka kwa Katibu wa Sera na Uenezi wa Tawi la CCM Moscow Ndg. KOLOA KASSIM, (+79260327055).
4. Kamati ya Siasa Imeaigiza Sekretarieti ya Tawi  chini ya idara yake ya SERA NA UENEZI, kusimamia na kuhamasisha wanachama wa  chama cha mapinduzi kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi  hili muhimu la Uchukuaji form na Uchaguzi wa Viongozi wa Tawi letu  kwa kuzingatia misingi ya CCM.
5. Kamati ya Siasa ya Tawi inawakumbusha wana chama wote ambao hawajapata Kadi za Uanachama , wakamilishe mchakato wa kujaza form ya kuomba Uanachama  na Picha 2 “passport size” , na kumkabidhi Ndg Kassim Koloa – Katibu wa Sera na Uenezi wa Tawi , ili waweze kupatiwa kadi ya Chama na ya Umoja wa Vijana UVCCM.
Mwisho, Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Tawi inatarajiwa kukutana wakati wowote kipindi cha Mwezi April 2012 ambapo pamoja na mambo mengine itatathimini utekelezaji wa maamuzi yake.  
                                                                         
Imethibitishwa na kutolewa na Ofisi ya Katibu wa Tawi;
MAKAO MAKUU, TAWI LA CCM MOSCOW.
SHIRIKISHO LA URUSI.
Email: ccmmoscow@gmail.com .                                            Website: ccmmoscow.blogspot.com.

0 comments

Post a Comment