Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Dr. Slaa kugombea Uraisi

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Dk Slaa atajwa Urais Chadema Send to a friend

Mussa Mkama
Drl Slaa
KAMATI kuu ya Chadema jana ilikutana jijini Dar es Salaam kujadili mambo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mkakati wa kumpata mgombea urais wa chama hicho baada ya mwenyekiti wake, Freeman Mbowe kuamua kugombea ubunge.
 
Habari kutoka kwa viongozi wa chama hicho zinasema kuwa mbunge wa Karatu, Dk Wilbroad Slaa ndiye anayeangaliwa zaidi kushauriwa kujitosa kwenye nafasi hiyo baada ya mjumbe wa kamati kuu, Profesa Mwesiga Baregu kugoma kugombea urais.
 
Tayari Dk Slaa ameshachukua fomu za kutetea kiti chake cha ubunge cha Karatu, lakini habari zinasema kuwa Chadema inamtaka katibu huyo mkuu kugombea urais baada ya kulichangamsha Bunge kwa hoja nzito katika vipindi vyake alivyolitumikia jimbo hilo.
 
Chadema, ambacho kimeongezeka nguvu katika kipindi cha miaka mitano baada ya kuingiza wanachama machachari ndani ya Bunge, imekuwa ikisaka mgombea urais ambaye ataweza kuendeleza umaarufu wa chama hicho na vyombo vya habari vimekihusisha chama hicho na mipango ya kumshawishi waziri mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye na Spika wa Bunge, Samuel Sitta kuingia kwenye mbio za urais kwa tiketi ya chama hicho.
Hata hivyo, taarifa za vyombo vya habari zimeeleza kuwa vigogo hao wawili wa CCM wamekataa kukiasi chama chao.
 
Katika uchaguzi mkuu uliopita, Mbowe alishika nafasi ya tatu kwenye harakati za kuingia Ikulu baada ya kufanya kampeni zilizogusa sehemu kubwa ya nchi, akitumia helikopta, lakini safari hii atagombea ubunge wa Jimbo la Hai.
Kama Dk Slaa atajitosa kugombea urais kwa tikei ya Chadema, CCM watakuwa wamepata mteremko wa kuchukua jimbo la Karatu ambalo wamekuwa wakilisaka kwa udi na uvumba.
 
Mkurugenzi wa Mambo ya  Nje wa Chadema, John Mnyika alikataa kuzungumzia kikao hicho na kueleza kuwa waandishi watapewa taarifa kamili leo.
“Baada ya kikao  kumalizika kesho, tutaitisha mkutano na waandishi wa habari... kitafanyika wapi na saa ngapi tutawajulisha usiku,” alisema Mnyika.
 
Tayari CCM imeshamteua mwenyekiti wakr, Jakaya Kikwete kuwa mgombea urais wakati CUF imemteua tena Profesa Ibrahim Lipumba kuwa mgombea wake.
 
Mwenyekiti wa TLP, Agustine Mrema naye hatagombea urais kwa tiketi ya chama hicho baada ya kuamua kurejea Vunjo kugombea ubunge. Mrema pia alishawahi kuwa mbunge wa Temeke..
Tags:

0 comments

Post a Comment