Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KITAIFA , HABARI ZA LEO - basi la HOOD lateketea kabisa. wanne wapoteza maisha

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
hivi ndivyo hali ilivyotokea baada ya basi la Hood lililokuwa likitoka Mkoani Mbeya kwenda Arusha,lilipogongana uso kwa uso na lori la mizigo lilolokuwa na mafuta ya kula tani 24 kutoka Morogoro kwenda Songea jana kwenye barabara iliyopo ndani ya hifandi ya Taifa ya Mikuki,mkoani Morogoro.watu watano walifariki na 41 kujeruhiwa.
Moto mkali ukiwaka mara baada ya magari hayo kugongana.
Basi la Hood lionekanavyo mara baada ya kuteketea kwa moto.
Dereva wa basi la Hood, Salehe Tembo ( 42) mkazi wa Mbezi , Jijini Dar es Salaam, akiwapelekwa chumba cha X –Ray kwa ajili ya kupigwa picha kabla ya kupatiwa matibabu baada ya kuungua sehemu mbalimbali mwilini.
Mama Asha Maneno akiwa na mwanae Milka Maneno , wakazi wa Wilaya ya Same, Mkoa wa Kilimanjaro wakiwa wodini baada ya kuumia sehemu mbalimbali za miili yao , katika ajali ya basi la Hood lililokuwa likitoka Mkoani Mbeya kwenda Arusha lilipogongana uso kwa uso na lori lililokuwa limebeba mafuta, eneo la mbunga ya wanyama ya Mikumi. 



0 comments

Post a Comment