Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KITAIFA , HABARI ZA LEO - KATIBU MKUU WIZARA YA NISHATI ASIMAMISHWA KAZI!

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo (pichani) amesimaishwa kazi! Akiongea na waandishi wa habari mjini Dodoma mapema leo, Katibu Mkuu Kiongozi, Philomon Luhanjo, alisema kuwa Jairo amesimamishwa kazi kuanzia kesho ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili zilizotolewa bungeni mapema wiki hii. Jairo anatuhumiwa kuandika barua ya kuchangisha fedha milioni 50 kwa idara 20 ili zitumike kushawishi wabunge wapitishe bajeti ya wizara yake. Haijaelezwa amesimamishwa kwa muda gani.

0 comments

Post a Comment