IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
Netanyahu ahidi kushughulikia matakwa ya waandamanaji
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameahidi kuyashughulikia matakwa ya waandamanaji ambao wamekasirishwa na kupanda kwa gharama za juu za maisha nchini Israel.
Akizungumza siku moja baada ya takriban watu laki moja kuandamana katika miji ya Tel Aviv na Jerusalem,Bwana Netanyahu amesema ataanzisha kikosi maalum cha kutathimini mabadiliko ya kiuchumi.
Amesema anaelewa hali halisi ya ugumu wa maisha inayowakabili waisrael wengi, lakini akaonya kuwa hatua za haraka zinaweza kuitumbukiza nchi hiyo katika mgogoro wa kiuchumi.
Wananchi wengi wa Israel wa hali ya kawaida wamekuwa wana shaka juu ya kupanda kwa bei, kutokuwepo kwa usawa wa kijamii pamoja na kodi kubwa.
Maandamano hayo hii leo yanatarajiwa kushika kasi zaidi ambapo wafanyakazi wa serikali za mitaa na wafanyakazi wa sekta nyingine wamepanga kufanya mgomo wa siku moja.
You Are Here: Home - HABARI ZA KIMATAIFA , HABARI ZA LEO - Maandamano yaanza ncini Israel kupinga kupanda kwa gharama za Maisha
0 comments