Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Mpango wa kutofanyika uchaguzi Zanzibar 2010 wadunukia

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

MWENYEKITI wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amepinga kauli ya msaidizi wa katibu mkuu wa chama hicho aliyesema kwamba CUF inaunga mkono kufutwa kwa uchaguzi wa rais Zanzibar mwaka huu ili Amani Abeid Karume aendelee kuwa madarakani kufanikisha uundaji wa serikali ya mseto.

Akizungumza na Mwananchi jana, Profesa Lipumba alisema msimamo wowote wa chama ni lazima upitishwe na baraza kuu la CUF.

Ismail Jussa, ambaye ni msaidizi wa Maalimu Seif na ambaye pia ni mkurugenzi wa mambo ya nje wa CUF, alinukuliwa na gazeti dada la Mwananchi la The Citizen toleo la juzi akisema kwamba msimamo wao ni kuona Rais Karume akiongezewa muda ili asimamie kikamilifu mchakato wa amani visiwani humo ambao tayari ameuanza.

"Sioni ubaya wowote wa kumuongezea muda (Rais Karume) ili amalize kazi aliyoianza," alisema Jussa. "Maridhiano ni jambo la muhimu zaidi kwa Wazanzibari kuliko uchaguzi."

Alitaja moja ya kigezo kuwa ni uhasama unaozuka kila uchaguzi unapofanyika hivyo kuufanya uchaguzi uonekane kwamba unawagawa Wazanzibari badala ya kuwaunganisha.

Lakini Profesa Lipumba alipinga kauli hiyo ya Jussa na kusema: "Sisi kama chama hatujawa na msimamo huo. Kulingana na katiba, baraza kuu la taifa ndilo lenye mamlaka ya kuamua na kutoa msimamo kama huo."

Aliendelea kusema: "Msimamo ambao hadi sasa baraza limeutoa na tunaendelea kuusimamia ni kuona kwamba Wazanzibar wote wanaandikishwa kwenye daftari la wapiga kura.รข€

Hata hivyo, Profesa Lipumba alisema Rais Karume akitoa msimamo huo, wako tayari kuujadili na kuutolea msimamo.

Tetesi kwamba Rais Karume anaweza kuongezewa miaka 10 ya kuiongoza visiwa hivyo vyenye siasa ya upinzani mkali, zilianza kuvuma miezi miwili ya mwishoni mwa mwaka jana.

Kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar, rais haruhusiwi kuendelea kuwepo madarakani au kugombea tena baada ya kuongoza visiwa hivyo kwa miaka 10 mfululizo iliyogawanyika katika vipindi vya miaka mitano ya uchaguzi.

Iwapo italazimu Rais Karume aendelee kuwapo madarakani, itabidi katiba ya Zanzibar ibadilishwe ili kujenga uhalali huo.

Kila mara uchaguzi unapokaribia kunakuwa na mapendekezo kama hayo yanayotolewa na wanasiasa kutaka rais aliye madarakani aendelee.

Wakati rais wa zamani, Dk Salmin Amour akikaribia kumaliza kipindi chake, kulikuwa na wazo kama hilo la kutaka aongezewe muda, lakini baada ya serikali kusema litashughulikiwa katika muda muafaka, lilizimika hadi wakati huu Karume anapomaliza muda wake.

Hata hivyo, safari hii hali imekuwa tofauti kidogo kutokana na pendekezo hilo kuungwa mkono na msaidizi wa kiongozi huyo wa CUF ambaye ana ushawishi mkubwa kwenye siasa za Zanzibar.

Jussa alitoa kauli hiyo katika kipindi ambacho Maalim Seif amekutana faragha mara mbili na Karume na kufuatiwa na tamko lake la kumtambua kiongozi huyo wa CCM kuwa mshindi wa kiti cha urais wa Zanzibar. Karume naye alijibu kwa kuteua wanachama wawili wa CUF kuwa wawakilishi, akiwa mwanasiasa machachari, Juma Haji Duni.

Vikao vya viongozi hao wawili wa kisiasa wa Zanzibar vimeelezewa na wote wawili kuwa ni kwa ajili ya maslahi ya wananchi wa visiwa hivyo. ilitokana na matumaini ambayo yameanza

Tags:

2 comments

  1. Anonymous says:

    Nimejaribu kuisoma taarifa yenye kichwa cha habari "MPANGO WA KUTOFANYIKA UCHAGUZI ZANZIBAR 2010 WANUKIA"lakini kwa bakhti mbaya naona maelezo ya makala yako hayakuzungumzia huo mpango wa kutofanyika uchaguzi bali umeguzungumzia nukta nyengine kabisa,tafadhali kuwa makini na makala zako.
    nawasilisha.

  2. Anonymous says:

    Nimejaribu kuisoma taarifa yenye kichwa cha habari "MPANGO WA KUTOFANYIKA UCHAGUZI ZANZIBAR 2010 WANUKIA"lakini kwa bakhti mbaya naona maelezo ya makala yako hayakuzungumzia huo mpango wa kutofanyika uchaguzi bali umeguzungumzia nukta nyengine kabisa,kuwa makini na makala zako.
    nawasilisha.

Post a Comment