Washukiwa wa Maumau mwaka 1952 |
Wizara ya mambo ya nje pamoja na ofisi ya Jumuiya ya Madola zilisema haziwezi kubeba jukumu hilo kisheria, lakini jaji anayesikiliza shuri hilo alitupilia mbali hoja hiyo.
Jaji huyo amesema hajaona kama kulikuwa na utesaji wowote, lakini kama ulikuwepo, serikali ya Uingereza ndio ilikuwa na mamlaka.
Shauri hilo litaruhusu kufunguliwa kwa kesi ya tuhuma za ukatili uliofanywa dhidi ya vuguvugu la Maumau kati ya mwaka 1952 hadi 1961.
Waliowasilisha shauri hilo ni Ndiku Mutwiwa Mutua, Paulo Muoka Nzili, Wambugu Wa Nyingi na Jane Muthoni Mara, ambao umri wao ni kati ya miaka 70 hadi 80.
Katika shauri hilo, awali, jaji aliambiwa kuwa Bw Mutua na Bw Nzili walihasiwa, Bw Nyingi alipigwa hadi kupoteza fahamu katika tukio ambalo watu 11 walipigwa hadi kufa, huku Bibi Mara akinyanyaswa kijinsia. Lakini ofisi ya mambo ya nje ilisema jukumu la kisheria lilikabidhiwa kwa jamhuri ya Kenya baada ya kupata uhuru wake mwaka 1963.
0 comments