Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia FFU wakiwa wameimarisha ulinzi katika kituo cha polisi kati ambako anashikiliwa Mbowe.
Gari maalum la kikosi cha kutuliza ghasia likiwa limeegeshwa tayari kusubiri amri ya kamanda wa polisi kuwatawanya wafuasi wa Chadema.
Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi ACP, Faustine Shirigile akiongea na baadhi ya viongozi kuhusiana na hatima ya kukamatwa kwa Mbowe.
Wafuasi wa Chadema wakiondolewa kituoni hapo.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof Ibrahim Lipumba akifika katika kituo cha polisi kati kwa nia ya kumdhamini Mbowe lakini hadi tunaenda mitamboni alikuwa hajafanikiwa.
KUFUATIA kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendele (Chadema), Freeman Mbowe wafuasi wa chama hicho walifika katika kituo cha polisi kati leo asubuhi kupinga kitendo cha kiongozi wao huyo kukamatwa.
Akiongea na waandishi wa habari mbunge wa Chadema Jimbo la Ubungo, John Mnyika alisema: "kimsingi mwenyekiti wetu hakupaswa kukamatwa kwa kigezo kuwa kakaidi amri ya Mahakama, maana alifanya mazungumzo kuhusu kutohudhuria mahakamani siku hiyo. Kitendo hiki kinaonyesha kuwa kuna shinikizo kutoka sehemu fulani."

0 comments