IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
SERIKALI imesema kuwa ipo katika mchakato wa kukamilisha sera ya elimu, ambapo kwa shule za awali mwanafunzi atasoma kwa mwaka mmoja na shule za msingi atasoma kwa miaka sita badala ya saba.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Muluga, alisema hayo hivi karibuni alipokuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kongamano la elimu, linalofanywa na Shule Kuu ya Elimu kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 50, tokea kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Waziri Muluga alisema kuwa mchakato huo, unafanywa baada ya kugundua wanafunzi wanamaliza shule za msingi wakiwa na umri mkubwa.
Mbali na hilo, Muluga alizindua shahada ya pili ya ualimu kwa masomo ya jioni.
Kwa mujibu wa waziri huyo, UDSM imekuwa ikipiga hatua kubwa kwa kuanzisha digrii hiyo, ambayo itawawezesha wananchi wengi wanaobanwa na kazi zao kuweza kujifunza.
Kwa upande mwingine, mhadhiri wa shule hiyo ya elimu, Profesa Justinian Galabawa, alishauri kuwa kuna umuhimu wa kuongeza ubora wa walimu hapa nchini, kwa kufanya hivyo elimu itaweza kuwa bora.
Alishauri walimu ni lazima wapende kujifunza kwa kusoma kila siku ili wawazidi wanafunzi na wawe na maarifa zaidi.
You Are Here: Home - HABARI ZA KITAIFA , HABARI ZA LEO - Shule ya msingi kuishia darasa la sita
0 comments