Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA LEO - Wapigadebe Ubungo wafungwa miezi 3 jela

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi wa Sokoine Drive (Jiji) mkoani Dar es Salaam imewahukumu kifungo cha miezi mitatu jela wakazi wanne wa mkoani humo kwa madai ya kupiga debe na kusababisha usumbufu kwa abiria katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Ubungo, Dar es Salaam.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu wa Mahakama hiyo, William Mtaki baada ya washitakiwa hao kukiri kosa hilo mahakamani hapo, suala ambalo ni kinyume na kifungu No. 16 (1) na (2) cha sheria ndogo ndogo za Jiji la Dar es Salaam iliyotungwa kwa ajili ya Kituo cha Mabasi cha Ubungo.

Waliohukumiwa kifungo hicho ni pamoja na Shaaban Muya (21) mkazi wa Sinza, Abdul Rajab (25) na Samora Mohammed (35), wakazi wa Kimara pamoja na Meshack Mwalingo (35), mkazi wa Gongo la Mboto.

Awali Mwendesha Mashitaka wa Mahakama hiyo, John Kijumbe, alidai mahakamani hapo kuwa mnamo Aprili 19 mwaka huu katika Stendi ya Mabasi ya Ubungo, washitakiwa hao kwa pamoja walikutwa wakipiga debe na hivyo kuwabughudhi abiria.

Alidai kuwa, huku wakitambua wazi kufanya hivyo ni kinyume na sheria na taratibu zilizowekwa na Jiji zinazowakataza kufanya hivyo, wao walikaidi agizo hilo na kuendelea na shughuli hiyo kwa makusudi ambapo alimwomba hakimu kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia hiyo.

Kutokana na kosa hilo Hakimu Mutaki alitoa adhabu ya kifungo cha miezi mitatu jela au kulipa faini ya Sh 50,000 kwa kila mmoja ambapo walishindwa kulipa fedha hizo na hivyo kwenda jela kutumikia kifungo.

0 comments

Post a Comment