Askari mwandamizi wa Marekani, Adm Mike Mullen, alisema vita nchini Libya "vitadumu muda mrefu", licha ya mashambulio ya anga kutoka kwa majeshi ya Marekani na majeshi ya umoja wa nchi za kujihami za Ulaya Nato kuharibu asilimia 30-40 ya majeshi ya ardhini ya Libya.
Marekani imeruhusu utumiaji wa ndege za kivita zisizokuwa na rubani kama silaha kwani zina " uwezo mkubwa wa kulenga shabaha kuliko ndege za kawaida"
Waasi wa Libya wamekuwa wakipambana na majeshi ya Kanali Gaddafi tangu mwezi Februari lakini inaonekana wameshindwa kusonga mbele.
Adm Mullen pia alisema hapakuwa na dalili zozote za upinzani wa Libya kuungwa mkono na al-Qaeda.
Akizungumza na majeshi ya Marekani nchini Iraq, alisema makundi yenye siasa kali huenda yakajiingiza katika ghasia hizo, lakini akaongeza: "Tuko macho, na makini kweli na sijaona dalili zozote za makundi hayo. Kusema ukweli, sijaona alama zozote za kuwepo al-Qaeda huko."
0 comments