Kiongozi wa kanisa Katoliki Baba Benedict wa 16 hapo jana aliongoza siku takatifu ya Ijumaa kuu inayoadhimishwa na wakristo kote ulimwenguni.
Kiongozi huyo wa dini ambaye ni mzaliwa wa Ujerumani, aliongoza msafara wa msalaba kama ilivyofanyika siku za kale, na akawakumbusha waumini jinsi matamanio ya dunia, kama vile hamu ya kufanikiwa, yanaweza kuwafanya watu kupoteza utu wao. Katika sala yake ya ufunguzi, Baba Benedict pia alitaja mateso yanayowakabili vijana na wanyonge, pasi na kutaja moja kwa moja hali ya kufichuka kwa kashfa ya unyanyasaji watoto kingono uliokuwa ukifanywa na mapadri uliozuka katika miaka ya hivi karibuni.
Maelfu ya watu, wengi wakiwa wamebeba mishumaa, walilizunguka eneo la Colosseum, kupitia vituo 14 vya msafara wa msalaba.
0 comments