WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amewataka wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini
kuacha siasa na kuwa wavumilivu katika kutatua matatizo yao na kuacha tabia za migomo na
maandamano.
Aidha, amesema matokeo ya matatizo hayo ni juhudi za Serikali katika kuongeza udahili wa wanafunzi hao ambapo kuna changamoto nyingi.
Akizungumzia tatizo la rasilimaliwatu nchini na migomo inayoendelea katika vyuo vikuu, alisema Serikali inaendelea kukabiliana na matatizo ya miundombinu na fedha inayotokana na Bodi ya Mikopo ambayo inalalamikiwa mara nyingi.
“Wanafunzi hawa ambao ni wataalamu wanaotazamiwa nchini wanatakiwa kuacha siasa kutatua matatizo yao, bali watumie hoja na Serikali inajitahidi kutatua matatizo
yao,” alisema.
Alisema wanatakiwa kujipanga kutatua matatizo yao na si kufanya uamuzi kama wanasiasa badala ya kujijengea uwezo wa ndani katika kuwasilisha malalamiko yao.
Alisema mbali na changamoto hizo za migomo kwa wanafunzi, lakini baada ya miaka mitano Tanzania itakuwa na rasilimaliwatu wa kutosha ambao watasaidia kuondoa utegemezi kwa wataalamu wa nje.
Akizungumzia changamoto katika elimu ya sekondari na msingi, alisema kinachotakiwa sasa ni kupunguza kasi ya ujenzi wa miundombinu na kuboresha iliyopo na mahitaji ya msingi kama maabara, madawati na mengineyo, kwa miaka mitano ijayo.
Alisisitiza kuwa katika kukabiliana na changamoto ya walimu kwa shule za sekondari wanaendelea kuongeza udahili ambapo baada ya miaka hiyo, kutakuwa na walimu 20,000 wa Sayansi na 20 wa masomo mengine kutoka chuokikuu cha Dodoma pekee.

0 comments