Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Baada ya kumshambulia muuza kitimoto sasa watoa mikongoto kwa walokole

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Suala la ubaguzi wa dini unaendelea kushamiri katika Mkoa wa Morogoro ambapo vurugu za kidini zikiripotiwa kutokea eneo la Mto wa Mbu hivi karibuni, leo asubuhi kijana mmoja ameingia matatani baada ya kukunjwa na mzee mmoja kwa kile kilichosemekana kuhubiri neno la Mungu barabarani jambo lililomkera mzee huyo ambaye aligoma kutaja jina lake.

Tukio hilo limetokea leo majira ya saa tatu asubuhi katika barabara ya Makongoro iliyopo katikati ya Mji wa Morogoro, ambapo kijana huyo Inocent Hamad, alimua kuwahubiria watu mbali mbali waliokuwa wakipita katika barabara hiyo yenye msongamano mkubwa wa watu.

Ikumbukwe kuwa hivi karibuni MKUU wa Wilaya ya Morogoro, SAIDI  Mwambungu, alitoa amri  kuzuia kuuzwa kwa nyama ya nguruwe (kitimoto) kwa muda katika baa ya mkazi mmoja inayojulikana kama Baa ya Kimario iliyopo mtaa wa Makaburi (B) Kata ya Mji Mpya mjini hapa kufuatia wananchi wa dini ya Kiislamu wanaoishi katika mtaa huo kulalamika kwa mkuu huyo kwamba moshi wa kitimoto unaotoka katika jiko la baa hiyo iliyopo jirani na makazi yao  ni kero.

Inocent ambaye hivi karibuni kabla ya kuokoka alikuwa ni miongoni mwa vijana waliokuwa wakivuta bangi na kuosha magari katika kijiwe kilichopo jirani na ofisi za CCM wilaya ya Morogoro zilipo kando kando mwa barabara hiyo ya Makongoro na mwandishi wa habari hii ni miongoni mwa watu walioshangazwa na kitendo cha  kumuona kijana huyo aliyekuwa kibaka wa kutupwa katika eneo hilo kubadilika na kuwahubiria wenzake kubadilika na kuacha maisha ya uporaji na uvutaji bangi.

"Nimekuja hapa kijiweni kuwaeleza habari njema vijana wenzangu kama mnavyojua mimi nilikuwa mwanachama mzuri sana hapa kijiweni, lakini kwa sasa Mungu ameniokoa na kunifumbua hivyo nimemua kuja hapa kuwaeleza kwamba maisha haya mnayoishi hapa ya kuvuta bangi na kupora watu mwisho wake ni Jehenamu. Nafasi mnayo sasa yakubadilisha maisha yenu kama ambavyo nimefanya mimi ambaye kwa sasa naishi maisha ya amani na upendo tofauti na awali nilivyokuwa hapa kijiweni" alisikika Inocent akiwaeleza vijana waliokuwa kijiweni hapo, lakini hata hivyo vijana hao walionekna wakimbeza na kumfananisha na mtu aliyechanganyikiwa kimaisha.

Wakati vijana hao wakionekana kumbeza, Mzee mmoja alijitokeza na kumzuia Mlokole huyo kuhubiri injili katika eneo hilo, akidai kwamba hana kibali cha kufanya mkutano katika barabara hiyo, lakini Inocent alimjibu kuwa hafanyi mkutano wa siasa bali ana hubiri neno la Mungu. "Mimi nawahubiria watu neno la Mungu unaponizuia kufanya kazi ya Mungu ni sawa na kupingana  na Mungu aliyenipa mamlaka ya kufikisha neno lake kwa watu wake," alisema Inocent.

Katika hali ya kushangaza mzee huyo baada ya kuelezwa maneno hayo yaliyoonekana kumchoma, aliamua kumkwida Mlokole huyo lakini umati wa watu uliokuwepo eneo hilo uliingilia kati na kumzonga mzee huyo ambaye alimwachia Inocent.

Alipotakiwa kuzungumza na mtandao huu, Mzee huyo aligoma na kuamua kutimua mbio huku akiwa ameshikilia mfuko wake wa Rambo na baada ya mzee huyo kuondoka umati huo wa watu ulimpongeza kijana huyo amabaye licha ya kukunjwa na mzee huyo hakuonjesha dalili yoyote ya hasira na kwamba badala yake alionekana akicheka.

Alipohojiwa na mwandishi wetu Inocent, alisema kuwa baba yake mzazi Mzee Kalumed Hamad ni Muislam na mama yake ni RC na kwamba yeye ameokoka hivi karibuni alipokuwa akiosha magari la Mlokole mmoja wa Kanisa la Calvary Assembles of God lililopo kando kando ya barabra ya SUA eneo la Kikundi.

"Kaka wewe unanijua vizuri nilikuwa hapa naosha magari na kuvuta bangi lakini Mungu ameniokoa na kuokoka kwangu kumeigawa familia yangu ambapo mpaka leo baba hakupenda mimi kuokoka lakini najua baba wa hapa duniani hana nguvu zaidi ya baba Mkuu wa Mbinguni", alisema Mlokole huyo mwenye msimamo mkali.


Tags:

0 comments

Post a Comment