WAKATI suala la kuwashwa mitambo ya Dowans likiwa halijulikani, sasa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, imesema taarifa ya mikakati ya muda mefu na mfupi kukabili kero hiyo, iliyopendekeza itatangazwa na Spika wa Bunge, Anna Makinda.
Nchi ipo katika tatizo kubwa la mgawo wa umeme na kusababisha kuwapo kwa msuguano wa kutaka mitambo ya Kampuni ya Dowans, iwashwe kwa haraka kupunguza mgawo huo au isiwashwe.
Wafanyabiashara wengi, wamiliki wa viwanda na wasomi wanataka kuwashwa kwa mitambo hiyo, huku baadhi ya wananchi wakipinga hatua hiyo.
Hata hivyo, Kamati ya Bunge inayoongozwa na Januari Makamba iliyokuta jijini Dar es Salaam jana kwenye ofisi ndogo za Bunge na watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), ilikamilisha majuimuisho ya mapendekezo ya ripoti hiyo.
Jana, Makamba alisema kamati yake itakabidhi ripoti hiyo, ofisi ya Bunge na kwamba ndio itakayokuwa na mamlaka ya kutangaza au kutoitangaza ripoti hiyo.
“Pamoja na mambo mengine, kanuni za Bunge ndizo zinatutaka kufanya hivyo,’’ alisema Makamba.
Hata hivyo, kwa mujibu wa chanzo chetu huenda ripoti hiyo ikatangazwa leo.
Wakati huo huo, habari zimeeleza kuwa mitambo ya Dowans inaweza kuwashwa wiki hii.

0 comments