BAADA ya kutoa hutoba ya mwezi kuelezea mambo mbalimbali kuhusu taifa, Rais Jakaya Kikwete amekwenda Paris, Ufaransa ambako atatoa mada kuhusu uwazi na uwajibikaji katika sekta ya madini na gesi asilia.
Tanzania ni moja ya nchi duniani ambayo ina rasilimali nyingi za madini ikiwemo tanzanite ambayo hayapatikani sehemu yoyote duniani. Hata hivyo, mikataba mingi iliyosainiwa chini ya Sheria ya Madini ya mwaka 1998 ni ya siri na imetajwa kutonufaisha nchi huku ikigubikwa na harufu ya ufisadi.
Jana, Ikulu ilitoa taarifa ambayo imeweka bayana nafasi hiyo ya Rais kutoa mada hiyo ikisema mkutano huo una malengo ya kuongeza uwazi na uwajibikaji katika mapato yanatokanayo na uchimbaji wa madini, mafuta na gesi asilia.
''Rais Kikwete anatarajiwa kutoa mada juu ya shughuli za uziduaji na uwazi katika mapato ya madini katika mkutano wa kimataifa wa tasnia ya uziduaji ambayo ina malengo ya kuongeza uwazi na uwajibikaji katika mapato yatokanayo na uchimbaji madini, mafuta na gesi asilia (EITI),'' ilifafanua Ikulu.
Katika taarifa hiyo, Ikulu ilifafanua kwamba, Tanzania iliomba kupewa uanachama wa muda wa EITI tangu mwaka 2009 na kuongeza: ''Tanzania itaweza kupata uanachama kamili baada ya kuwa imekamilisha na kutimiza vigezo na kuweka misingi ya utoaji taarifa hizo muhimu kwa umma juu ya malipo ya kodi kutoka makampuni mbalimbali yaliyopo nchini.''
Ikulu iliongeza kwamba lengo la kujiunga na EITI ni kuongeza uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa rasilimali za madini, mafuta na gesi asilia kwa kutangaza hadharani malipo yanayotokana na rasilimali zake kwa manufaa ya wananchi.
''Utaratibu huu utaweka wazi na kuondoa usiri ambao unaweza kuwa mwanya wa kuficha mapato halisi ya makampuni husika,'' ilisema taarifa ya Ikulu na kuongeza kwamba baada ya kumalizika mkutano huo wa Paris, Rais atasafiri kwenda Nouckhott, Mauritania kuhudhuria kikao cha marais wa Afrika wanaosaka suluhisho la tatizo la kisiasa nchini Ivory Coast.
Akiwa nchini humo, Rais atajiunga na Marais wa Afrika Kusini, Burkina Faso, Nigeria, Chad na Equatorial Guinea pamoja na wawakilishi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi-ECOWAS.

0 comments