Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - UDSM wamvamia Waziri Kawambwa

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
GARI alilokuwamo Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa jana lilinusurika kuvunjwa vioo baada mawe na chupa kurushwa kufuatia ujio wake kuonekana kushindwa kutatua madai ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Wanafunzi hao ambao walikuwa wameungana na wenzao kutoka Chuo Kikuu Kishiriki (DUCE) walikusanyika katika eneo la Uwanja wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani kumsubiri Waziri huyo aliyetarajia kujibu hoja nne zilizohusu madai yao.

Alipofika katika eneo la uwanja wa mpira, wao wakitokea katika viwanja maarufu vya 'Revolutionary Square', Waziri alikaribishwa kwa nyimbo mbalimbali hasa kama zile za 'kama sio juhudi zako Nyerere na Kawambwa angesoma wapi' huku wengine wakimtaka asizungumze kisiasa suala hilo badala yake atoe tamko la namna gani watapata Sh 10,000.

Wanafunzi hao walinyamaza na kumsikiliza Waziri, ambaye alianza kwa kusema "Nimekuja kuwasikilia kwa hiyo naomba mnipe matatizo yanayowakabili, nipo hapa kwa ajili yenu mnaweza kuanza kuniambia matatizo hao "Lakini hamjambo? aliwauliza Waziri " wanafunzi hao walimjibu "Njaa hali mbaya."

Ndipo zilipoanza kutolewa hoja na wanafunzi hao ikiwamo ile ya ongezeko la fedha za kujikimu kutoka Sh 5,000 za sasa hadi hadi 10,000, Serikali itoe fedha za dharura kwa wanafunzi wote kiasi cha Sh 100,000 kwa ajili ya kujinusuru na njaa hadi hapo mitihani ya kumaliza muhula itakapomalizika mwezi wa tatu mwaka huu.

Madai mengine yaliyotolewa na wanafunzi hao ni kumtaka Waziri huyo wa elimu kutoa tamko la kufuta kesi inayowakabili wanafunzi wenzao waliokamatwa Ijumaa ya wiki iliyopita wakishinikiza Serikali kusikia madai yao.

Akijibu hoja hizo, Dk Kawambwa alisema kuwa Serikali imekwishapokea malalamiko na hoja zao, lakini maombi hayo hayawezi kutekelezeka hadi ipitishwe bajeti ijayo ya Serikali jambo lililowafanya wanafunzi hao kupandisha jazba na kumtaka ashuke kwenye jukwaa aondoke kwa kile walichokieleza kuwa alikuwa akipiga siasa.

Wanafunzi walifikia hatua hiyo baada ya mwanaharakati chuoni hapo, Rich Mwita kusimama na kumweleza waziri kuwa alikuwa hajaeleweka na kumtaka atoe majibu ya mwisho ili wao waweze kuona hatua za kuchukua.

Waziri akawajibu kwa kifupi kuwa kesi zilizoko mahakamani hana uwezo wa kuzifuta sababu ule ni mhimili mwingine, kuhusu ongezeko la Sh 5,000 ili kufikia Sh 10,000 akawaambia Serikali imekubali.

Kuhusu kiwango cha Sh10,000 alisema hadi hazina ifanye ukokotoaji na kuhusu fedha za dharura akasema kiwango hicho ni kikubwa na hakiwezi kupatikana kwa dharura.

Kutokana na kauli hizo, wanafunzi walipandwa na jazba na ndipo walipozidi kupiga kelele za kumtaka ashuke na aondoke katika eneo hilo.

Hata hivyo, wanafunzi hao walimuuliza maswali ambayo Waziri alionekana kuyakwepa kujibu na kuonekana kuwa na hofu kutokana na jazba walizozionesha wanafunzi hao.

Aliposema kuwa suala la malipo ya posho kutoka sh 5000 hadi 10,000 lisubiri bajeti ya mwaka ujao walimuuliza kuwa "Mbona suala la Dowans halikusubiri bajeti sasa iweje suala letu linasubiri bajeti?,"walihoji wanafunzi hao.

Swali lingine aliloulizwa Waziri ni kwamba kipindi cha uchaguzi kuna baadhi ya wafanyakazi waliongezewa mishahara bila kupitisha kwenye bajeti nalo hakulijibu "Unasema mpaka bajeti ipitishe nyongeza hiyo mbona kipindi cha uchaguzi baadhi ya wafanyakazi waliongezewa mishahara fedha zilitoka wapi?," walihoji.

Dk Kawambwa alifunga mkutano huo na kuondoka bila kuafikiana na wanafunzi hao hali hiyo ilileta uvunjifu wa amani kwa kuwa wanafunzi walirusha chupa za maji na mawe na kuwapiga askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU).

Wanafunzi watano wazirai
Baada ya kurushiwa mawe na chupa za maji hali ilibadilika chuoni hapo kwani askari walijihami na kurusha mabomu ambapo wanafunzi watano walizirai papo hapo na kubebwa kupelekwa katika zahanati ya chuo hicho bila kujitambua.

Wanafunzi hao walimwambia Waziri kuwa hadi sasa hawana fedha za kumaliza muhula na kumuomba atoe ufafanuzi wa kuweza kuwasaidia hadi kumaliza muhula huku wengine wakisikika wakiongea kwa sauti "Njaa inatuua, tunaomba utunusuru" walisikika wakitoa sauti.

Wakizungumza mbele ya Waziri, wanafunzi hao walisema kuwa hawaendi nyumbani wala chuo hakitafungwa ila wanataka fedha hiyo ipatikane haraka iwezekanavyo vinginevyo waliahidi kujipanga upya na kuhakikisha wanafika Ikulu.

"Tunaongea mbele yako mheshimiwa Waziri kama utaweza kutupa majibu yanayojitosheleza tutajipanga vizuri na kuhakikisha tunafikisha kilio chetu sehemu husika maana unaonekana umeshindwa kutuweka wazi," alisema Rich Mwita mwenyekiti wa wanaharakati.
Tags:

0 comments

Post a Comment