SPIKA wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda leo amekataa ombi la Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, aliyeomba Bunge liache shughuli zake za kawaida ili lijadili milipuko ya mabomu iliyotokea katika kambi ya Jeshil la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ), Gongo la Mboto, Dar es Salaam.
Baada ya Spika Makinda kumaliza kuomba dua ya kuiombea nchi yetu na kuliombea Bunge, Lissu aliomba mwongozo wa Spika na akatoa ombi hilo.
Katika maelezo yake, Mbunge huyo ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bugeni alisema, taifa lipo kwenye msiba mkubwa hivyo akaomba Bunge lijadili maafa hayo kama jambo la dharura.
Lissu aliomba Bunge kutengua kanuni ya 47 na 48 na kwamba alitumia kanuni ya 150 (1) inayomruhusu Mbunge kuomba kutengua kanuni yoyote kwa madhumuni mahsusi.
Kanuni ya 47 ya Bunge inaliruhusu Bunge kuacha shughuli zake ili kujadili jambo la dharura na muhimu kwa umma.
Spika wa Makinda alimjibu Lissu kwa kusema kuwa, jambo hilo linaweza kufanyika baada ya kipindi cha maswali na majibu na kama jambo hilo ni la dharura, halisi na lenye maslahi kwa umma.
Amesema, Bunge haliwezi kuijadili milipuko hiyo kwa kuwa, si jambo la dharura, na ndiyo maana hata jana Bunge liliahirisha shughuli zake kwa kuwa taifa lipo kwenye msiba tangu mabomu yalipuke usiku wa kuamkia jana, na hakukuwa na shughuli za Bunge jana ili kutoa fursa kwa viongozi kushughulikia maafa hayo.
Amesema, Kamati ya Ulinzi na Usalama inaondoka leo Dodoma kwenda Dar es Salaam kushughulikia madhara ya milipuko hiyo iliyosababisha vifo vya watu 26 na kujeruhi zaidi ya raia 300.
Makinda ameagiza sehemu ya posho za wabunge za jana zikatwe ili kuwachangia waathirika wa milipuko hiyo iliyoanza juzi saa mbili usiku na kumalizika jana alfajiri.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amesema, licha ya kuua na kujeruhi watu wengi, mabomu hayo yamesababisha hasara kubwa ya mali za wananchi na taifa kwa ujumla.
Kwa mujibu wa Pinda, hadi jana jioni taarifa zilionesha kuwa, milipuko hiyo imeua watu 20, imejeruhi watu 315, 135 kati ya hao wamelazwa hospitalini.
“Tunaomba wananchi wote wawe watulivu na warejee kwenye maeneo yao wakati Serikali inashughulikia tatizo hilo” amesema Pinda bungeni mjini Dodoma wakati anatoa hotuba ya kuahirisha mkutano wa pili wa Bunge.
“Maafa haya ni yetu sote Watanzania. Waliopoteza maisha na mali zao ni ndugu zetu, hivyo nawaomba Watanzania wote ndani na nje ya nchi popote walipo, na washirika wetu wa maendeleo kuisaidia serikali kukabiliana na tatizo hili”amesema Waziri Mkuu.
Amewapa pole waliokumbwa na maafa hayo na ameomba Watanzania waungane kumuomba Mungu azipokee peponi roho za marehemu na kuzilaza mahala pema.

![](http://www.blogger.com/img/icon18_edit_allbkg.gif)
0 comments