Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Sakata la Mabomu Goongo la Mboto

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
(1) Upinzani: Mwinyi, Mwamunyange mjiuzulu
(2) Wanawake, watoto wahangika usiku kucha kuokoa maisha yao
(3) Waingia Gereza la Seregea kukwepa mabomu Dar
(4) **Hakuna askari aliyekufa**



KAMBI ya Upinzani Bungeni, imewataka Waziri wa Ulinzi, Dk Hussein Mwinyi na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange, wajiuzulu.
Rai hiyo inafuatia milipuko ya mabomu iliyotokea juzi katika maghala ya kuhifadhia silaha katika kambi ya JWT Gongo la Mboto, jijini Dar es Salaam.
Wakiongea kwa nyakati tofauti mjini Dodoma jana baada ya kuahirishwa kwa kikao cha Bunge kufuatia mlipuko
mndahimu wa kambi ya upinzani Tundu Lissu, Waziri wa Ulinzi kivuli Joseph Selasini(Chadema) walitoa maoni hayo
huku Agustino Mrema (TLP) akisema inafaa mtu kuwajibika kwa tukio hilo na Hamad Rashid (CUF) akitaka serikali
ichukue hatua hukusu mabomu yaliyobakia.

Aidha, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Edward Lowassa akieleza kusikitishwa na tukio hilo na kutaka vyombo vya ulinzi na usalama kuachiwa vilifanyie kazi tukio hilo.Akizungumza kwa niaba ya kiongozi wa kambi ya upinzani, Tundu Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashriki.

alisema  serikali isiishie katika kutoa pole kwa walioathirika na badala yake, iwataka viongozi hao wa shughuli za ulinzi, wajiuzulu."Yapo mambo ya kujiuliza katika tukio hilo. Kwanza, kwa nini limetokea miaka miwili tangu lilipotokea tukio la milipuko ya Mbagala. Kwa nini silaha zihifadhiwe karibu na makazi ya  watu na kwa nini watu wajenge karibu na kambi za jeshi,"alisema Lissu akihoji.

Aliongeza kuwa anahisi tukio hilo inawezekana kuwa lilipangwa na kwamba alitegemea tukio la Mbagala  lingekuwa fundisho kwa serikali na JWTZ.

Lakini, akitoa alichokiita taarifa rasmi ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Waziri kivuli wa Ulinzi, Joseph Selasini
aliwaambia waandishi  kuwa kambi hiyo imeshtushwa na tukio hilo na inawataka Dk  Mwinyi na Jenerali Mwamunyange wawajibike kisiasa na kupisha uchunguzi huru wa tukio hilo
la mlipuko.


ULIKUWA ni usiku wa giza, simanzi, hofu na mtikisiko baada ya wananchi wa maeneo jirani na Kambi ya Jeshi Gongolomboto, waliposhuhudia vipande vya mabomu vikisafiri angani mithili ya vimondo.

Mwanga mkubwa wa moto ulitanda katika anga, kuanzia Gongolomboto, Kipawa, Jeti Lumo, Yombo Vituka –Yombo, Uwanja wa Ndege, Yombo Sigara na viunga vyake.

Jumatano Februari 16, usiku kuanzia saa 1;30  zilianza kusikika ngurumo mithili ya radi. Wengi waliamini ni radi kutokana na Jiji la Dar es Salaam kwa siku mbili kukumbwa na mvua kubwa, zilizoambatana na radi, upepo na ngurumo.

Hisia za radi ambazo ziliathiri miundombinu ya umeme zikawa zimetanda vichwani kwa watu, lakini kadri muda ulivyokuwa ukisonga, anga la maeneo hayo, liligubikwa na mwanga wa milipuko na vipande vya mabomu vikisafiri angani.

Awali, saa 2:00 usiku nikapigiwa simu na Mhariri wangu Denis Msacky akinitaarifu kufuatilia tukio hilo, na nikiwa njiani kukaribia na Tazara nilikutana na misururu mikubwa ya kina mama na watoto wakikimbia kutoka maeneo ya Gongo la Mboto huku wakionyesha ukosefu wa matumaini ya maisha.

Mfumo wa usafiri ulivurugika barabara ya Nyerere. Wakati nikishangaa kuwapo kwa  giza maeneo ya nyumbani kwetu, ghafla nikaona makundi ya watu hasa kina mama na watoto, wakiwa na vifurushi mikononi na migongoni yakipita kuelekea Tandika, Mbagala na Uwanja wa Taifa.

Redio zilikuwa zikitangaza watu wajifiche  mabondeni, nami muda wa saa tatu nikawa nimelala chini ya nyasi katika bonde nikilinda nyumba huku familia yangu, nikiwa nimeipeleka mbali na nyumbani. Nilala bondeni kwa saa nne, huku mji ukiwa umetulia huku mirindimo ya makombora, ikisikika jijini Dar es Salaam.

Kila mara nilijaribu kuwasiliana na Waziri wa Ulinzi Dk Hussein Mwinyi, aliwataka wananchi kuchukua tahadhari.

Lakini, mnamo saa 4:30 usiku  milipuko na vipande vya mabomu vilivyokuwa vikisafiri angani mithili ya vimondo, vilianza kupungua na hata anga likawa shwari.

Makundi ya watu ambayo tayari yalikwishafika Uwanja wa Taifa, Mbagala na Tandika, yalianza kurejea tena eneo la Yombo kupita katika njia hiyo, saa 8:00 usiku, misururu ya kina mama na watoto, ilionekana tena.  

Tags:

0 comments

Post a Comment